YANGA WAJIONDOA KWENYE MICHUANO YA KAGAME CUP | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, June 9, 2019

YANGA WAJIONDOA KWENYE MICHUANO YA KAGAME CUP

  Malunde       Sunday, June 9, 2019

Uongozi wa Klabu ya Yanga umeuandikia barua Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) sambamba na Shirikisho la soka Nchini (TFF) kujiondoa kwenye michuano ya Kagame inayoatarajiwa kuanza mapema mwezi ujao nchini Rwanda.

Mapema wiki iliyopita, CECAFA waliwaandikia barua Yanga ya kuwaalika kwenye michuano hiyo ambapo uongozi wa Yanga ulikuwa unasubiri kauli ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Zahera Mwinyi kama watashiriki au la.

Yanga wameandika barua hiyo wakielezea sababu mbalimbali za kujiondoa kwao kwenye michuano hiyo ikiwemo kumalizika kwa mikataba kwa wachezaji wao wengi.

Awali Uongozi wa Klabu ya Simba ulishafanya maamuzi na kuamua kujiondoa kwenye michuano hiyo ila kwa upande wa mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam wao wamethibitisha kushiriki.

Michuano ya Kagame inatarajiwa kuanza Julai nchini Rwanda ikishirikisha timu mbalimbali kutoka Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post