KANISA KATOLIKI LATOA WARAKA MZITO KUHUSU USHOGA


 Kanisa Katoliki duniani limetoa waraka wa mwongozo unaopinga dhana ya kisasa juu ya utambulisho wa jinsia asili.

Mwongozo huo wenye kurasa 31 za mafundisho, umetolewa leo Jumanne June 10, ukiwa na kichwa cha taarifa ''Mungu aliumba Mke na mume''

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ujerumani (DW), mwongozo huo unaozungumzia mzozo wa mafundisho umeongeza mjadala wa sasa kuhusu kupotosha dhana asilia ya kijinsia na kuyumbisha familia.

Waraka huo ambao umetolewa wakati wapenzi wa jinsia moja wakiendelea na sherehe za mwezi wa kujivunia jinsia zao, umekosolewa na makundi ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadilisha jinsia zao LGBT.

Hata hivyo, waraka huo haukutiwa saini na Papa Francis mwenyewe, lakini uliinukuu kauli yake na maandiko ya biblia kuhusiana na jinsia zilizoumbwa na Mungu kulingana na kanisa katoliki.

Aidha, waraka huo unatoa wito wa kuwapo kwa mazungumzo, lakini unatoa mwongozo juu ya masuala kadhaa yakiwamo yanayohusu jamii ya watu wanaobadilisha jinsia yao.

Vile vile, unakosoa vikali uelewa wa kisasa kuhusu jinsi na kusisitiza kwamba kuna mwanaume na mwanamke pekee.

Waraka huo umeendelea kusema kuwa nadharia za kisasa "zinapinga maumbile halisi na badala yake linakuwa ni suala la hisia za binadamu.

Unaongeza kuwa, utambulisho wa jinsia mara nyingi hauna msoingi wowote isipokuwa ni dhana potofu ya mkanganyiko wa uhuru wa hisia za mtu na vile anavyotaka yeye kuonekana na kutambulika.

Waraka huo unaendelea kusema kuwa jinsia haiamuliwi na watu binafsi bali ni Mungu pekee, "maandiko matakatifu yamefichua busara ya Mungu ya mtindo wake wa uumbaji ,ambaye alimpatia binadamu kazi ya mwili, kazi ya mwanamme na mwanamke."

Hata hivyo, waraka huo unasema kwamba watoto na vijana wanapaswa kufundishwa kumuheshimu kila mtu ili asiwapo atakayeumizwa na matusi au ubaguzi wa aina yoyote ile

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527