TUME YA MADINI IPO TAYARI KUKUSANYA BILIONI 475


Na Issa Mtuwa “WM” – Tunduru, Mbinga na Iringa 
Tume ya madini imesema ipo teyari kukusanya bilioni 475 katika mwaka wa fedha 2019/20 kama walivyopangiwa na serikali na kufikia malengo ya ukusanyaji kama ilivyofikia mwaka 2018/2019 ya kukusanya billion 310 ambapo malengo hayo ilivuka. 


Akiongea kwa nyakati tofauti akiwa wilayani Tunduru, Songea na Mbinga na Iringa Mwenyekiti wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amesema hayo wakati wa vikao  vyake na viongozi wa mikoa, wilaya, maafisa madini wa kaazi, viongozi na wachimbaji wadogo na wanunuzi wa madini kwenye maeneo yao akisisitiza kila mmojja kwa nafasi yake kuwajibika katika suala la usimamizi na ulipaji wa maduhuli ya serikali ili wafikie lengo hilo.  


Amesema serikali imeipangia Wizara ya Madini kukusanya jumla ya Tshs. bilioni 475 na wakusanyaji wa fedha hizo ni Tume ya madini na ili ifikie lengo la kukusanya kiwango hicho lazima wajipange kwa kila mdau anae husika kwa namna moja au nyinge awajibike kutimiza wajibu wake. 


“Ndugu zangu mkisoma jukumu namba moja la Tume ya madini ni kukusanya maduhuli ya serikali, pili kutatua migogoro ambayo ikiachwa inaathiri ukusanyaji wa maduhuli, pamoja na majukumu mengine lakini haya mawili ndio hasa yanayotufanya tuzunguke nchi nzima kuhimiza haya masuala.  


Tume tumesema, ili tufikie haya malengo kila ofisi ya Afisa Madini mkazi iseme imejiwekea malengo ya kukusanya kiasi gani na kila baada ya kipindi gani atakuwa amekusanya kiasi gani, na lazima kila ofisi ifikie hayo malengo. Pamoja na ofisi zetu ofisi zetu kusimamia makusanyo naombeni viongozi wa mikoa na wilaya wasaidieni watu wetu wanapo hitaji msaada wenu kwani tunajenga taifa moja. amesema Prof. Kikula. 


Akisisitizia hoja hiyo mwenyekiti amesema haya yote yanaweza kufikiwa kirahisi kwa kuunganisha nguvu zetu sote na kuzingatia mambo matatu, uwajibikaji, uadilifu hasa kuepuka rushwa na kufuata sheria. Ameongeza kuwa endapo kila mdau kwa nafasi yake atazingatia haya itakuwa rahisi kufikia lengo walilopewa. 


Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini Prof. Abdulkarim Mruma ameongeza kuwa jambo lingine la msingi ni lazima kila ofisi ya tume ya madini mikoa yote lazima iwe na mpango kazi unao onesha utaratibu wa utekelezaji wa majukumu kipindi kwa kipindi ili isaidie kujifanyia tathmini kuona ulikotoka, ulipo na unako elekea na muda uliobaki nao katika kufanikisha malengo ya mwaka 


Amesema bila kuwa na mpango kazi inaweza kuwa ngumu kufikia malengo yoyote hata haya ya ukusanyaji wa maduhuli, kwa hiyo amewasisitiza watumishi wa tume kuwa na mpango kazi ambao utawaonyesha kipindi hadi kipindi atakusanya kiasi gani cha maduhuli na kwamba hicho kinaweza kuwa kigezo kikubwa cha upimaji wa utendaji kazi kwa Maafisa Madini wakazi wa Mikoa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post