TRUMP ASAINI VIKWAZO VIPYA NA VIKALI DHIDI YA IRAN


Rais Donald Trump wa Marekani hapo jana amesaini amri ambayo amesema inaiwekea vikwazi vipya na vikali zaidi Iran. 

Vikwazo hivyo vitamlenga zaidi Kiongozi wa Kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei pamoja na maafisa wengine wa Iran, ikiwa ni pamoja na makamanda wanane wa ngazi za juu wa jeshi la walinzi wa mapinduzi ya Kiislamu nchini humo. 

Trump amesema ingawa Marekani haitaki vita na Iran, lakini adhabu hizo za kifedha zinahitajika ili kuiongezea shinikizo serikali ya taifa hilo. 

Rais huyo wa Marekani amesema Iran haiwezi kuruhusiwa kuwa na silaha za nyuklia. Uchumi wa Iran tayari ulikuwa umeathirika kutokana na vikwazo vya Marekani, ambavyo vilikuwa vimeinuliwa chini ya makubaliano ya kinyuklia ya mwaka 2015. 

Hata hivyo msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Abbas Mousavi amesema vikwazo hivyo havina athari yoyote kwa uchumi wa Iran.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post