TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE


Paris St-Germain wameipatia ofa Man United ya kubadilishana na mshambuliaji wa Brazil Neymar, 27, kwa kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba. (Independent)
Arsenal itahitaji nusu ya fedha zao ilizotengewa dirisha la uhamisho kumnunua beki wa Celtic raia wa Uskochi Kierna Tierney mwenye umri wa miaka 22 huku mchezaji huyo akiwa na thamani ya £25m kutoka kwa mabingwa hao wa Uskochi.. (Telegraph)

Hatma ya kiungo wa kati wa Croatia Mateo Kovacic, 25, katika klabu ya Chelsea haijulikani huku mkopo wake katika klabu ya Real Madrid ukitarajiwa kukamilika tarehe mosi mwezi Julai. Klabu hiyo ya Stamford Bridge bado haijamuongezea kandarasi. (Goal)

United itaimarisha hamu yao ya kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, 19, iwapo watamuuza Pogba. (Sun)

Neymar hatoruhusiwa kurudi katika klabu yake ya zamani Barcelona kutoka PSG hadi atakapoomba msamaha kwa mabingwa hao wa Uhispania na mashabiki wake na kukubali mshahara wake kupunguzwa (El Mundo - in Spanish)

Real Madrid haitakubali maombi ya chini ya 47.7m kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Dani Ceballos, ambaye amevutia hamu ya klabu ya Tottenham nchini Uingereza. (AS- in Spanish)
Spurs inachunguza kinda wa Denmark Andreas Skov Olsen, ambaye anaichezea klabu ya FC Nordsjaelland na ana thamani ya £15m. (Mirror)

Arsenal wanakataa ofa kutoka AC Milan kumuuza kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira, 23. (Mirror)

The Gunners wana hamu ya kumsajili winga wa klabu ya Dalian Yifang Yannick Carrasco, lakini bado hawajawasilisha ofa yoyote kwa mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 25 (Football.London)
Mkufunzi mpya wa Juventus Maurizio Sarri ana hamu ya kumsajili beki wa kulia wa Tottenham Kieran Trippier, 28, kama mchezaji ambaye anamlenga sana lakini anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Napoli ambao tayari wamewasiliana na mchezaji huyo.. (Mirror)

Mshambuliaji wa Real Madrid na Colombia James Rodriguez, ambaye alihudumu misimu miwili kwa mkopo akiichezea Bayern Munich, hana uhakika iwapo atasalia katika klabu hiyo ya Bernabeu msimu ujao. (Marca)

Newcastle United haina haja na mshambuliaji wa West Brom na Venezuela Salomon Rondon - ambaye alihudumu msimu uliopita akiichezea klabu hiyo ya ligi kuu ya Uingereza - licha ya uamuzi wa mkufunzi Rafael Benitez kuondoka katika klabu hiyo. (Star)

Aston Villa inataka kumnunua beki wa klabu ya Luton Town na Uingereza James Justin huku klabu ya Leicester pia ikiwa na hamu ya mchezaji huyo. (Birmingham Chronicle)

Beki wa klabu ya Manchester United na Uingereza Axel Tuanzebe, 21, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Aston Villa anataka hakikisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Sun)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal Dominik Szoboszlai, 18, anafikiria kuondoka katika klabu ya Red Bull Salzburg, huku Barcelona na Borussia Dortmund zikimnyatia mchezaji huyo wa Hungary. (Football.London)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post