TETESI ZA SOKA ULAYA ALHAMISI


Manchester United imejiondoa katika harakati ya kutaka kumsaini beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire baada ya kuambiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atagharimu £100m. (Mirror)
Mkufunzi wa klabu ya Nice nchini Ufaransa Patrick Vieira, 43, Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard, 39, kocha wa Manchester City Mikel Arteta, 37, wameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi Rafael Benitez. (Telegraph)

Raia wa Uhispania Mikel Arteta ameungwa mkono kuchukua ukufunzi wa klabu ya Manchester City wakati kocha Pep Guardiola atakapoondoka katika klabu hiyo. (Evening Standard)
Mikel Arteta

Mkufunzi wa klabu ya Burnley Sean Dyche pia analengwa na Newcastle lakini the Magpies watalazimika kuwalipa Burnley £10m kama fidia. (Daily Mail)

Manchester United itakutana na ajenti wa kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes, 24, ili kujaribu kumrai kuhamia katika klabu hiyo kwa dau la £70m kutoka klabu ya Sporting Lisbon. (O Jogo, via Talksport)

Juventus imeitaka kampuni ya vifaa vya michezo Adidas kuisaidia kifedha ili kuweza kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Corriere dello Sport - in Italian)

Manchester City iko katika mzungumzo na Juventus kuhusu usajili wa beki wa kulia wa Ureno Joao Cancelo. (Tuttomercato, via Star)

Kiungo wa kati wa Arsenal na Uruguay Lucas Torreira, 23, anasema kuwa AC Milan haijawasiliana naye kuhusu uhamisho katika klabu hiyo ya Serie A. (Talksport)

Bayern Munich imefanya mazungumzo na Paris St-Germain na ajenti wa mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Sepp van den Berg, anatarajiwa kujiunga na Liverpool kutoka kwa klabu ya PEC Zwolle. (Evening Standard)

Beki wa klabu ya Huddersfield Town na Uingereza Tommy Smith, 27, ananyatiwa na Stoke City pamoja na mabingwa wa ligi ya Uskochi Celtic. (Huddersfield Examiner)

Reading wanamnyatia winga wa Brazil Wenderson Galeno, 21, kwa mkopo kutoka Porto.(Futebol365)

CHANZO.BBC SWAHILI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post