RC MAKONDA APEWA AGIZO LA KUTAFUTA NYUMBA NA OFISI ZILIZOTUMIWA NA WAPIGANIA UHURU


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametakiwa na Waziri wa Mambo ya  Nje na Uhusiano wa Afrika Mashariki,  Profesa Palamagamba Kabudi kuzitafuta na  kuzitambua nyumba na ofisi zote zilizotumiwa na wapigania uhuru katika nchi mbalimbali za Afrika zilizopo Tanzania.

Profesa Kabudi ametoa agizo hilo leo, wakati akizungumza na wamiliki na wakuu wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.

“Wakuu wa nchi 16 watahudhuria mkutano huu na kuleta  ombi maalumu kufanya kumbukizi ya Nyerere watakapokuwa. Hii ni fursa kwetu kuweka kumbukumbu na ku identify (kutambua) maneno yote ambao wapigania uhuru wa nchi mbalimbali walikaa.”

“Tupitie nyumba zote walizokaa mfano Jacob Zuma (rais mstaafu wa Afrika Kusini) aliishi hapa,  Sam Nujoma (Rais mstaafu wa Namibia) na wengine wengi tuzitambue hizo nyumba na ofisi zao,” amesema Profesa Kabudi.

Aidha alisema kuwa Agosti 17, 2019  Tanzania itakuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) , ugeni aliodai pamoja na mambo mengine utafanya kumbukizi ya Julius Nyerere, Rais wa kwanza wa Tanzania.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post