AMUUA MWANAYE KISHA KUMPIKA KAMA SUPU GEITA | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 22, 2019

AMUUA MWANAYE KISHA KUMPIKA KAMA SUPU GEITA

  Malunde       Saturday, June 22, 2019
Picha haihusiani na tukio

Katika hali inayositaajabisha na kuacha maswali mengi, mwanamke mmoja mkazi wa Kitongoji cha CCM,Kijiji cha Buligi Kata ya Senga Wilayani Geita, Happiness Shadrack (36), anayedaiwa ni mgonjwa wa akili, amemuua mwanaye wa kumzaa, Martha Yakobo (1), kwa kumkatakata vipande vidogovidogo kisha kumuweka ndani ya sufuria na baadaye kumpika kama kitoweo/supu.  • Tukio hilo limetokea jana Ijumaa 7majira ya saa saba za mchana,muda mfupi baada ya mtoto aliyeuawa kupelekwa kulazwa kwenye chumba cha bibi yake, kama dada wa marehemu anavyosimulia ambaye amedai kuwa alikwenda kumlaza ndani na yeye kwenda kucheza nje, baada ya muda mfupi alimuona mama yake akiwasha jiko na kudai kuwa alikuwa akichemsha maji.

Kaimu Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Kamishina msaidizi wa polisi Dismas Kisusi akithibitisha kwa njia ya simu kuwepo kwa tukio hilo amesema kuwa tayari mhusika amefikishwa kituo cha polisi na upelelezi unaendelea.
Chanzo- EATV
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post