SIMBA SC WADONDOSHA MSHAMBULIAJI KUTOKA BRAZIL



Klabu ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa miaka miwili na mshambuliaji Wilker da Silva Raia wa Brazil.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa klabu hiyo umemtambulisha mchezaji huyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la usajili katika klabu hiyo Bingwa Tanzania Bara.

Huyu anakuwa ni mchezaji wa pili Raia wa kigeni kunaswa na Wekundu wa msimbazi baada ya jana kuingia mkataba wa mwaka mmoja na Kiungo Bora Barani Afrika kutoka klabu ya Al Hilal ya Sudan Sharaf Eldin Shiboub Ali
Abdalrahman 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527