SIMBA SC KUFUNGUA UWANJA MISUNGWI


Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu 2018/19 Simba SC wanatarajia kucheza mchezo wa kirafiki wilayani Misungwi Mwanza,ukiwa ni mchezo maalum wa ufunguzi wa uwanja wa Gwambina.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi kupitia ukurasa wake wa Instagram inasema kuwa “Tumealikwa kwenda kufungua Uwanja wa Gwambina uliopo Misungwi,Mwanza Timu itatua Mwanza kwa Ndege tarehe 20 Juni,2019” imeeleza taarifa hiyo. 

Mchezo huo maalum utapigwa katika uwanja wa Gwambina tarehe 21 Juni 2019 dhidi ya wenyeji Gwambina FC . 

Mabingwa hao ligi kuu soka Tanzania Bara wameahidi kushusha kikosi kamili kilichosheheni wachezaji wapya wa ndani ambao watavaa Uzi mwekundu kwa mara ya kwanza,Huku pia wakiwaomba wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi siku hiyo ya Mchezo “Wanasimba wa Kanda ya Ziwa jiandaeni Kuipokea timu yenu” ilimalizia Taarifa hiyo. 

Hii itakuwa Ziara ya kwanza kwa timu hiyo mara baada ya kufanikiwa kutetea Taji lake la Ligi kuu Soka Tanzania Bara Baada ya kumaliza ligi wakiwa na alama 93,huku Yanga wakishika nafasi ya pili kwa alama 86 na Azam fc wakimaliza katika nafasi ya tatu kwa alama 75. 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post