SERIKALI YASHAURIWA KUUNGANISHA TAASISI ZOTE ZENYE MAJUKUMU YANAYOFANANA IKIWA NI PAMOJA NATBS, OSHA NA TFDA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma

Kamati ya bunge ya bajeti imeishauri serikali kuhakikisha inaunganisha taasisi zote zenye majukumu yanayofanana ikiwa ni pamoja na TBS, OSHA, TFDA na Fire ili kuondoa kero na usumbufu kwa wafanyabiashara

Hayo yamesemwa  Juni 17,2019 bungeni jijini Dodoma na mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Bajeti George  Simbachawene  wakati akiwasilisha taarifa ya kamati ya bajeti kuhusu hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2018 na mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2019/20 pamoja na  tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya serikali  kwa mwaka 2018/20 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya serikali  kwa mwaka 2019/20.

Mhe.Simbachawene amesema ilikurahisisha utekelezaji katika maeneo mbalimbali ni vyema kuunganisha taasisi hizo ili kuondoa kero  na usumbufu unaojitokeza    pindi taasisi hizo zinapotembelea na kufanya ukaguzi  kwenye viwanda mbalimbali hapa nchini.

Aidha,Mhe.Simbachawene amesema pamoja na nchi yetu kuwa na Rasilimali kubwa ya mifugo  na samaki  bado haijaweza kunufaisha wananchi na taifa kwa ujumla hivyo ni wakati umefika kuacha kujipongeza kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo na badala yake kujielekeza kuongeza kasi ya kutumia Baraka hizo kwa kunufaisha watu wa Taifa la Tanzania Pamoja na kunufaisha sekta ya kilimo.

Kuhusu suala la Madini Mhe.Simbachawene amesema bado kuna tatizo kwa baadhi ya wafanyabiashara  kutorosha dhahabu kwenda nje ya nchi kwani kiwango cha kilo 600 za dhahabu  zilizouzwa katika soko la Geita  ni kidogo.

Wakichangia maoni juu ya taarifa ya bajeti kuu ya serikali baadhi  ya wabunge akiwemo mbunge wa Sumve Kwimba Richard Ndassa wamesema kuna haja kubwa  ya serikali kuangalia  upya sekta ya kilimo hususan Soko  ili kuinua wanyonge.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527