SERIKALI YAPELEKA BIL 8 JIJI LA TANGA KUTEKELEZA MIRADI YA AFYA NA ELIMU

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kulia akiwa kwenye kikoa cha baraza la madiwani maalum la kujibu hoja za mkaguzi wa serikali CAG la Jiji hilo kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi


 Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akifuatiwa na Naibu Meya wa Jiji hilo Mohamed Haniu
 Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji akizungumza wakati wa kikao hicho kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji hilo Alhaji Mustapha Selebosi
 DIWANI wa Kata ya Msambweni Jijini Tanga (CUF) Abdurahamani Mussa akichangia wakati wa kikao hicho
Sehemu ya Madiwani wa Jiji la Tanga wakifuatilia kikao hicho
Serikali imepeleka kiasi cha sh Bil 8 kwa Halimashauri ya Jiji la Tanga kwa ajili ya kutekeleza miradi ya Maendeleo kwenye sekta za Afya na elimu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigela wakati wa baraza la madiwani maalum la kujibu hoja za mkaguzi wa serikali CAG la Jiji Hilo lilofanyika hapo Jana.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha wanatekeleza miradi ya Maendeleo kwa wakati ili kumaliza kero zinazowakabili wananchi.

"Mnachotakiwa Halimashauri ni kuhakikisha fedha hizo zinatumika katika malengo yaliyokusudiwa lakini na miradi hiyo iweze kuzingatia thamani halisi ya fedha hizo"alisema RC Shigela.

Awali akisoma hoja za CAG Mwekahazina wa Jiji la Tanga Corner Sima alisema kuwa ucheleweshaji wa fedha kwa ajili yautekelezaji wa miradi ya kimkakati yamajiji nchini umesababisha kushindwa kutekelezeka .

"Ucheleweshaji wa fedha hizo ilisababishia kuibua hoja kutoka kwa CAG kwani katika sh Bil 232.5 zilizotumwa kwa ajili yamiradi tuliweza kutumia sh Bil 4.7 sawa naasilimia 2% ya fedha hizo"alisema Sima..

Hivyo ofisi ya CAG imeielekeza Halimashauri ya Jiji hilo kuwasilisha mpango kazi wa matumizi ya fedha hizo na namna ambavyo zitaweza kutumika katika kutekeleza miradi hiyo ya kimaendeleo.

Nae Mstahiki Meya wa Jiji hilo Seleboss Mustafa alisema kuwa katika mwaka huu wa fedha wamejipanga kusimamia kwa ukaribu mapato pamoja na kuibua vyanzo vipya.

Huku akitilia mkazo namna walivyojipanga kuhakikisha wanatoa mikopo yenye masharti nafuu kwa makundi maalum ya vija a ,wanawake na Walemavu walioko katika kata 21 za Jiji hilo.

"Tumekuja na hari ya kuhakikisha tunamaliza changamoto za kimaendeleo kwa wananchi wetu huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni ukusanyaji wa mapato ili kutekeleza miradi yetu ya Maendeleo na kuwaondolea adha wananchi wetu"alisema Meya huyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527