MKUU WA WILAYA ATANGAZA KUWEKA DORIA KUDHIBITI WANAOFANYA UCHAWI NJIA PANDA KAHAMA MJINI


SALVATORY NTANDU

Serikali wilayani Kahama imesema itaweka ulinzi katika njia panda inayoelekea katika nyumba ya mkuu wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambayo inatumika kufanyia vitendo vya ushirikina baada ya kukithiri kwa vitendo vya kishirikina katika eneo hilo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake baada ya kuongezeka kwa matukio hayo na kusema kuwa wataweka walinzi maalum katika eneo hilo ili kuwabaini watu wanaotekeleza vitendo hivyo.

Amesema mbali na kufanya vitendo hivyo ambavyo havifai kwenye jamii wahusika wamekuwa wakiharibu barabara na mazingira kwa kutupa vitu mbalimbali katika eneo hilo pindi wanapomaliza kufanya kafara zao kama vile nazi,kuku,mbuzi hali ambayo haitaweza kuvumilika.

Amefafanua kuwa jamii inapaswa kuachana na vitendo hivyo vya upigaji wa ramli chonganishi hivyo ni budi wakafanya kazi halali za kuwapatia vipato halali na kuachana na imani potofu za kishirikina zinazofanywa na waganga wakienyeji katika eneo hilo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post