Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (kulia), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, akizingumza wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD inayochapisha magazeti ya Tanzanite, Fahari ya Tanzania na Tanzania Perspective jijini Dar es Salaam Juni 14, 2019 ikiwa ni
mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari ili kukuza ushirikianona kutangaza shughuli za Mfuko huo mpya ambao ulianzishwa baada ya serikali kuunganisha Mifuko mine ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (kulia), akiwa na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi, akizingumza wakati alipotembelea chumba cha habari cha kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD inayochapisha magazeti ya Tanzanite, Fahari ya Tanzania na Tanzania Perspective jijini Dar es Salaam Juni 14, 2019
ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari ili kukuza ushirikiano na kutangaza shughuli za Mfuko huo mpya ambao ulianzishwa baada ya
serikali kuunganisha Mifuko mine ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunis Chiume (kushoto), akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD
inayochapisha magazeti ya Tanzanite, Fahari ya Tanzania na Tanzania Perspective, Bw.Evans Magege wakati Meneja huyo alipotembelea chumba cha habari cha magazeti hayo jijini Dar es Salaam Juni 14, 2019 ikiwa ni mwendelezo wa ziara
yake ya kutembelea vyombo vya habari ili kukuza ushirikianona kutangaza shughuli za Mfuko huo mpya ambao ulianzishwa baada ya serikali kuunganisha Mifuko minne ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF, PPF na GEPF.
Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Umma, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF), Bi. Eunice Chiume (watatu kushoto), akiwa na Afisa Uhusiano
Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw. Abdul Njaidi,(wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na waandishi wa gazeti hilo.
***
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
THAMANI ya Mfuko mpya wa Hifadhi ya Jamii
kwa Watumishi wa Umma, (PSSSF) imefikia Shilingi Trilioni 5.8 baada ya uamuzi wa serikali kuunganisha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni PSPF, LAPF NA PPF.
Meneja Kiongozi Uhuasiano na Elimu kwa Umma wa Mfuko huo, Bi/ Eunice Chiume ameyasema hayo leo Juni 14, 2019 wakati alipotembelea ofisi za kampuni ya CZ Information and Media Consultant LTD inayochapisha magazeti ya Tanzanite,
Fahari Yetu na Tanzania Perspective jijini Dar es Salaam ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari ili kukuza ushirikiano na kutangaza shughuli za Mfuko huo mpya.
“Mfuko wetu ni mkubwa sana tangu zoezi hili la kuunganisha Mifuko likamilike, tuko vizuri na tunatoa huduma kupitia ofisi zetu nchi nnzima Bara na Visiwani”,
alisema Bi. Cheume.
Alisema, wanachama wa PSSSF wanapaswa kutambua kuwa majukumu makuu ya Mfuko yamebaki kuwa yale yale ambayo ni kuandikisha wanachama, kukusanya michango ya kila mwezi ambapo asilimia 15 inatoka kwa mwajiri na asilimia 5 kutoka kwa mfanyakazi, lakini pia kulipa pensheni kwa wastaafu.
“Takwimu zetu zinaonyesha hadi sasa tuna wastaafu wanaopokea pensheni 124,500 na kati ya hao hadi kufikia wiki moja iliyopita wastaafu elfu 10,500 bado hawajahakiki
taarifa zao kama sheria na kanuni zinavyoelekeza na nitumie nafasi hii kuwahimiza wastaafu wote ambao bado hawajahakiki taarifa zao wafanye hivyo”, alifafanua.