Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo shirika la AGAPE ACP la mkoani Shinyanga linalojihusisha masuala ya utetezi haki za wanawake, vijana na watoto, kuwawezesha watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI, kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa vijana wameadhimisha siku ya mtoto wa Afrika katika kata ya Usanda.
Madhimisho hayo yamefanyika leo Juni 14, 2018 kwenye viwanja vya shule ya msingi Singita kata ya Usanda, ambapo kilele chake kinatarajiwa kufanyika June 16 mwaka huu, ambapo kimkoa yatafanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika inasema “Mtoto ni msingi wa taifa endelevu, Tumtunze, Tumlinde, na Kumuendeleza.”
Akizungumza, mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Kaimu Afisa elimu shule za msingi halmashauri ya Shinyanga Christina Bukori, akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewataka wazazi kutumia maadhimisho hayo kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto wao, bali wawalinde pamoja na kuwatimizia mahitaji yao ili kutimiza ndoto zao.
Amesema maadhimisho hayo ni kumbukumbu ya mauaji ya kikatili ambayo walifanyiwa watoto huko nchini Afrika Kusini mwaka 1976, ambapo walikuwa wakidai haki zao za msingi, na kuwataka wazazi wakajitafakari na kubadilika kuacha kunyanyasa watoto wao.
“Tanzania imekuwa ikiadhimisha siku hii ya mtoto wa Afrika miaka 28 mfululizo tangu mwaka 1991, kwa kutumia kauli mbiu mbalimbali ili kuhamasisha wazazi waweze kuwapatia watoto haki zao za msingi, ikiwamo kuwalinda, kuwaendeleza, na kutowabagua,”amesema Bukori.
“Hivyo nawataka wazazi kupitia maadhimisho haya, mjitafakari na kubadilika kuacha kunyanyasa watoto wenu kwa kuwafanyia vitendo vya ukatili, pamoja na kuwanyima haki zao ikiwamo elimu, kwa kuwaozesha ndoa za utotoni, na hatimaye kuzima ndoto zao,”ameongeza.
Naye Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, amesema matukio ya ukatili dhidi ya watoto kwenye halmashauri hiyo yamepungua, isipokuwa tatizo la mimba za wanafunzi bado limeendelea kuwa changamoto.
Amesema kwa takwimu za kuanzia Machi hadi Juni mwaka huu, kuna mimba sita, tano shule za sekondari na moja msingi, ambapo pia kuna tukio la ubakaji ambalo lipo kwenye uchunguzi, na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kurubuni wanafunzi bali wawaache watimize ndoto zao.
Kwa upande wake mratibu wa afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga, ambao wanatekeleza mradi huo kwenye kata hiyo ya Usanda, amesema wataendelea kushirikiana na serikali ili kumaliza matukio ya ukatili kwa watoto, likiwamo tatizo la mimba na ndoa za utotoni ambalo limeanza kupungua kwa kiasi kikubwa.
Nao baadhi ya watoto walioshiriki kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika akiwamo Irene Laurent, wameipongeza serikali pamoja na shirika hilo la Agape, kwa kuendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kwa wanafunzi, hali ambayo imewasaidia kujitambua na kuachana mapenzi katika umri mdogo.
TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Christina Bukori akimwakilisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika katika halmashauri hiyo yaliyofanyika kata ya Usanda na kuwataka wazazi kuacha kufanyia watoto vitendo vya ukatili, ikiwamo kuwaozesha ndoa za utotoni.Picha zote na Marco Maduhu - Malunde1 blog
Afisa maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Mhoja, akielezea hali halisi ya ukatili kwenye halmashauri hiyo na kubainisha kuwa umepungua isipokuwa tatizo la mimba za utotoni bado ni changamoto.
Mratibu wa mradi wa elimu ya afya ya uzazi na ujinsia kutoka Shirika la Agape Lucy Maganga akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya mtoto wa Afrika kiwilaya Shinyanga vijijini yaliyofanyika kata ya Usanda, na kuahidi Shirika hilo wataendelea kushirikiana na Serikali kumaliza matukio ya ukatili kwa watoto likiwemo tatizo la mimba na ndoa za utotoni.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ambapo kilele chake ni Juni 16.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi kutoka Shule ya Agape wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wazazi katika Kata ya Usanda wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kutakiwa kuwatimizia mahitaji watoto wao pamoja na kufuatilia maendeleo ya shuleni.
Wazazi katika Kata ya Usanda wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, wakisiliza uumbe mbalimbali za kulinda watoto wao na kuwatekelezea mahitaji yao.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yakiendelea kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yakiendelea kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yakiendelea kwenye halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi kutoka Agape wakitoa burudani kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi kutoka Agape wakiendelea kutoa burudani kwa kucheza ngoma ya asili kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Singita Kata ya Usanda nao wakitoa burudani ya kucheza ngoma kwenye maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Burudani ya ngoma ikiendelea kutolewa.
Wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Nzagaluba Kata ya Usanda wakitoa burudani ya kuimba nyimbo zinazohusu haki za watoto, kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Burudani za kukimbia kwenye magunia kwa upande wa wanafunzi wa kiume zikitolewa kwenye maadhimisho hayo ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Burudani za kukimbia kwenye magunia kwa upande wa wanafunzi wa kike zikitolewa kwenye maadhimisho hayo ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Washindi wa kukimbiza kuku kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wakiwa wameshikilia kitoweo na kisha kuondoka nacho mara baada ya kuibuka na ushindi.
Mgeni Rasmi kaimu Afisa elimu wa shule za msingi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Christina Bukori akitoa zawadi mbalimbali kwa washindi ambao waliibuka kwenye michezo mbalimbali katika siku hiyo ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika kwenye halmashauri hiyo.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi yakiwamo madaftari ,kalamu na sabuni.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi yakiwamo madaftari na kalamu.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi yakiwamo madaftari na kalamu.
Zawadi zikiendelea kutolewa kwa washindi.
Awali mgeni Rasmi akikagua bidhaa za makundi ya vijana wajasiriamali na kusikiliza maelezo namna walivyo anzisha vikundi hivyo pamoja na changamoto ambazo zinawakabili, kwenye maadhimisho hayo ya Mtoto wa Afrika na kuwataka waboreshe ubora wa bidhaa zao ili zipate kuwainua kiuchumi.
Mgeni rasmi alizindua zoezi la utoaji wa matone ya vitamini "A" kwa watoto wadogo ili kuboresha afya zao.
Awali wanafunzi wakiingia na maandamano kwenye maadhinisho hayo ya siku ya Mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maandamano yakiendelea.
Mgeni rasmi akipokea maandamano.
Mgeni rasmi akihitimisha maadhimisho hayo ya siku ya mtoto wa Afrika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kugawa unga wa lishe kwa akina mama 20 wa kata hiyo ya Usanda pamoja na kupiga nao picha ya pamoja na kuwataka wazingatie Lishe bora kwa watoto wao ili wapate kukua kiakili pamoja na kuwa na afya njema.
Na Marco Maduhu- Malunde 1 Blog