NDUGAI ASEMA KIONGOZI KIJANA WA SERIKALI HAJIELEWI...HAJITAMBUI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 26, 2019

NDUGAI ASEMA KIONGOZI KIJANA WA SERIKALI HAJIELEWI...HAJITAMBUI

  Malunde       Wednesday, June 26, 2019

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema kiongozi mmoja wa Serikali aliyezungumza maneno yasiyofaa kuhusu Bunge la Tanzania na wabunge na kumdanganya hadharani Rais John Magufuli kuwa wawakilishi hao wa wananchi wamewadhihaki wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, hajitambui.

Spika ametoa kauli hiyo bungeni  jana Juni 25, baada ya Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, (ACT-Wazalendo), kuomba muongozo kwa kutumia kanuni ya 68 (7), kuhusu jambo lililotokea mapema bungeni.

Zitto alilazimika kuomba muongozo huo baada ya Spika Ndugai kutoa ufafanuzi kwamba hakuna mbunge yeyote aliyewadhihaki wachezaji wa Taifa Stars baada ya mchezo wake na Senegal.

“Mheshimiwa Spika, kwa kutumia kanuni 68 (7), kuhusu jambo lililotokea bungeni mapema, umeelezea jambo ambalo limetokea nje ya bunge kuwa mmoja ya viongozi wa serikali kuwabagaza wabunge waliokwenda Misri.

Mara baada ya mbunge huyo kuomba muongozo huo, Spika Ndugai, alijibu akisisitiza kuwaomba wabunge kutolikuza jambo hilo.

“Naomba tusilikuze jambo hili kabisa, kama wabunge tungekuwa na mawazo kama wachezaji wanamakosa isingewezekana wabunge wengine 30 kwenda Misri. Ni bahati mbaya sana, kwamba tuna viongozi wa serikali, wanadiriki kumdanganya Rais hadharani.

“Kiongozi wa serikali unapoongea mbele ya Rais, jipange, ongea ukweli mtupu mbele ya Mwenyezi Mungu na sisi hatutamani kusema, natamani kufunguka kidogo…inatosha..inatosha.

“Nasema wazi bahati mbaya kijana wetu huyu hajitambui, hajielewi kwa sababu ana nguvu aliyonayo ana makundi ya vijana kwenye mitandao ambao wanaweza kumtukana Spika, lakini tuache,”alisema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post