MWANAMKE AUAWA AKITUHUMIWA KUIBA DEBE LA NYANYA SHINYANGA


Mwanamke aliyejulikana kwa jina la Esther Samwel (35) mkazi wa Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga ameuawa kwa kupigwa na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake na wananchi waliojichukulia sheria mkononi wakimtuhumu kuiba nyanya debe moja na nusu, mboga aina ya chinese mafungu sita na mahindi mabichi matatu.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Richard Abwao tukio hilo limetokea jana Jumatano Juni 19,2019 majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika maeneo ya Kitangili, kata ya Kitangili, tarafa ya Shinyanga Mjini, Manispaa na Mkoa wa Shinyanga. 

“Chanzo cha tukio hilo ni wananchi kujichukulia sheria mkononi baada ya kumtuhumu marehemu kuiba nyanya debe moja na nusu, mboga aina ya chinese mafungu sita na mahindi mabichi matatu”,amesema Kamanda Abwao.

Amesema juhudi za kuwatafuta na kuwakamata waliohusika na tukio hilo zinaendelea. 

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527