MTANZANIA MWINGINE KUJIUNGA NA TIMU YA MSUVA

Nickson Clement Kibabage anataraji kujiunga na Diffa Hassani El Jadida msimu ujao 2019/2020. 


Taarifa ya Klabu ya Mtibwa Sugar kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram inasema kuwa Kibabage ambaye anacheza katika nafasi ya Beki wa kushoto ameingia makubaliano ya miaka ya 4 kuitumikia Difaa El Jadida (2019-2023). 


Difaa Hassan El Jadida na Mtibwa Sugar Sc tayari wamekubaliana juu ya uhamisho huu wa Kibabage ambaye alibakiza mwaka mmoja wa kuitumikia Mtibwa Sugar Sc. Kibabage ameweka wazi ni kwanini ameamua kuchagua jezi namba 43 

"Nimechagua namba 43 kwasababu naiona namba yangu ya bahati, hii nimeivaa Mtibwa na nimefanya vizuri , Difaa walikuwa tayari kunipa namba nyingine lakini niliwaomba niendelee na hii ingawa walisisitiza iwapo Difaa itacheza michuano ya kimataifa CAF CL au CAF CC nitabadilishiwa namba sababu ya sheria ya michuano hii inahitaji namba 1-30 ktk Jersey " Kibabage

Klabu ya Difaa El Jadida sasa itakuwa na wachezaji wawili kutoka Tanzania akiwemo Saimon Msuva ambaye kwa sasa yuko nchini Misri katika Kambi ya Taifa Stars.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post