MKUU WA MAJESHI ETHIOPIA APIGWA RISASI


Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amefahamisha kuwa mkuu wa majeshi Seare Mekonen alipigwa risasi baada ya kuzuka machafuko Jumamosi jioni katika taifa hilo la Pembe ya Afrika. Hata hivyo hali ya mkuu huyo wa jeshi haijulikani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa shirika la habari la AFP,  Abiy alizungumza kupitia kwenye televisheni ya taifa akiwa amevaa mavazi rasmi ya kijeshi baada ya kutokea jaribio la mapinduzi katika jimbo la Amhara lakini maelezo zaidi hayakutolewa kuhusiana na lengo la mashambulio hayo katika jimbo la pili lenye watu wengi zaidi nchini Ethiopia linaloongozwa na Rais wa kikanda Ambachew Mekonen.

Ubalozi wa Marekani ulitoa tahadhari baada ya kusisikia milio ya bunduki katika mji mkuu wa Addis Ababa, na pia vurugu karibu na mji mkuu wa jimbo la Amhara, Bahir Dar.

Serikali ya Ethiopia imesema jaribio hilo la kuipindua serikali ya kikanda kaskazini mwa nchi hiyo lilishindikana. Ofisi ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed imelaani jaribio hilo la mapinduzi katika ujumbe wa Twitter uliochapishwa Jumamosi jioni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527