AMUUA KWA KUMKATA SHINGO MCHEPUKO WA MKEWE BAADA YA KUWAFUMANIA WAKIHONDOMOLANA

Maafisa wa polisi eneo la Trans Mara Magharibi kaunti ya Narok  nchini Kneya wamemkamata jamaa mwenye umri wa miaka 25 baada ya kupatikana na kosa la kumuua mwenzake aliyekisiwa kuwa mpenzi wa mkewe.

 Mathew Langat aliripotiwa kumuua Stanley Bor kwa kumkata shingo baada ya kumfumania akishiriki ngono na mkewe wa miaka 22 nyumbani kwake majira ya saa nne usiku Jumamosi Juni 22.

 Kisa hicho cha kushtua kimetokea katka kijiji cha Ng'endale, eneo bunge la Angata Barrikoi kule Trans Mara Magharibi.

 Akithibitisha kisa hicho, chifu wa kata ya Angata Barrikoi Paul Kirui alisema mshukiwa alimvamia marehemu kwa mkuki na kumdunga shingoni na kwenye koo.

 Mwili wa marehemu ulipelekwa katika mochuari ya hospitali ya Tenwek huku mshukiwa pamoja na mkewe wakitiwa mbaroni.

 Chanzo - Tuko

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527