KIGOGO WA CHADEMA AUAWA MOROGORO

Uongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro umeeleza kusikitishwa na kifo cha katibu mwenezi wa jimbo la Malinyi, Lucas Lihambalimu baada ya kudaiwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nyumbani usiku wa manane.

Akizungumza na Mwananchi jana, katibu wa Chadema mkoa wa Morogoro, Barnabas Okola alisema kwa mujibu wa taarifa walizopata watu wasiojulikana walifika nyumbani kwa Lucas saa 8:00 usiku na kumgongea.

Okola alisema alipofungua mlango ghafla alipigwa na kushambuliwa na watu hao kwa kumpiga risasi shingoni.

“Kihistoria Lucas hakuwa na ugomvi na mtu au watu alikuwa mpole na mchapa kazi ndani ya chama, tuliposikia ameuawa kila mtu alipigwa butwaa,” alisema.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527