WAHUNI WATUMIA JINA LA MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI (NEC) KUTAPELI WATU FACEBOOK | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, June 15, 2019

WAHUNI WATUMIA JINA LA MKURUGENZI WA TUME YA UCHAGUZI (NEC) KUTAPELI WATU FACEBOOK

  Malunde       Saturday, June 15, 2019

Kundi la matapeli linadaiwa kutumia jina la Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi nchini (NEC) Dk. Athumani Kihamia kwa lengo la kutapeli watu ili kujipatia fedha.


Akizungumza leo, Dk. Kihamia amesema kuna watu wamefungua akaunti feki ya mtandao wa kijamii wa facebook na  kuwatapeli watu kwa kuwatumia ujumbe wa maneno (Messenger), ambapo ametoa tahadhari kwa wananchi kua makini na utapeli huo unaoendelea.

“Kuna baadhi ya watu wamefungua akaunti kwa jina langu na kulitumia kwa kujipatia fedha kwa njia hiyo ya utapeli huku wakijua ni kosa kisheria, baadhi ya jumbe wanazotuma ni pamoja na kwamba Dk. Kihamia anauwezo wa kuwatafutia kazi katika mbuga ya Hifadhi ya Serengeti,”

“Yaani tayari kuna watu wameliwa fedha na hao matapeli hao kupitia sehemu ya ujumbe unaosema sema hivi “angalia kama kuna mtu amemaliza chuo na hajapata kazi uniambie maana kuna kazi shirika la Marekani la Thomson Zoology  kule Serengeti national park na wanahitajika watu wawili wenye diploma au degree kwa ajili ya kazi ya reservations na mshahara milioni moja na laki nane kama kuna mtu aniambie mapema nimpe namba ya huyo mzungu ahsante,” amesema.

Dk. Kihamia amesema aliishawahi kukanusha taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii lakini anaona hali inazidi kuwa mbaya hivyo amewataka wananchi kupuuza ujumbe huo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post