MAHARUSI VIKONGWE WAZUA GUMZO WAKIPEANA MABUSU MOTO MOTO WAKIFUNGA NDOA

Wachumba wazee kutoka kaunti ya Murang'a nchini Kenya wamewaacha waumini waliokuwa wamehudhuria harusi yao na kucheko baada ya kubadilishana mabusu moto moto wakati wakifunga ndoa mnamo Ijumaa, Juni 14,2019. 

Wawili hao ambao walionekana kuwa na umri wa takriban miaka 60 hivi walipanga kusherehekea ndoa yao kama njia moja ya kuwaonesha wanao kwamba mapenzi hayazeeki.

Harusi hiyo ilihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wakiwemo ndungu, jamaa, marafiki na majirani.

 Bi harusi alivalia rinda jeupe na kuonekana maridadi ajabu. Baada ya wawili hao kuvishana pete , mchungaji ambaye aliyekuwa akiwaunganisha wawili hao aliwaruhusu kubadilishana mabusu mbele ya umati uliokuwepo, na kuwaacha waliohudhuria ndoa hiyo na mshangao. 

Wawili hao walikuwa na wakati mzuri wakati wakifunga ndoa yao. 

Bwana harusi alibaki kuduwaa kama kwamba hakuwa amesikia alichoambiwa na ikamlazimu mchungaji kurejelea ujumbe wake kwa lugha ya Kikuyu na kusema "mumunya mundu". 

Papo hapo alimkamata mkewe na kuanza kumpa mabusu moto moto huku umati uliokuwepo ukiangua kicheko na kushangilia. 

Video hiyo aidha imesambaa kwa kasi mitandaoni huku watu wengi wakituma jumbe za kuwapongeza na kuwatakia kila la heri. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527