MAJAMBAZI YATELEKEZA SILAHA KAHAMA YAKIFUATILIWA NA POLISI | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 27, 2019

MAJAMBAZI YATELEKEZA SILAHA KAHAMA YAKIFUATILIWA NA POLISI

  Malunde       Thursday, June 27, 2019

NA SALVATORY NTANDU

Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linaendelea kuwatafuta Majambazi wawili waliotelekeza silaha aina ya Gobole iliyotengenezwa kienyeji,panga mmoja  pamoja na pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili MC 359 AZE baada ya kushindwa kutekeleza tukio la uporaji.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga (ACP) Richard  Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea jana katika mtaa wa shunu  saa tatu na nusu usiku ambapo walilenga kufanya uhalifu katika duka la M pesa  la Neema Byabato mkazi wa shunu wilayani Kahama.

Amesema wakati polisi wakiwa katika doria walipata taarifa za kuwepo kwa tukio hilo kisha kuanza kuwafuatilia  Majambazi hao walipobaini kuwa wanatafutwa  walianza kukuimbia na katika harakati za kukimbia walidondosha silaha hizo na  kisha kuitelekeza pikipiki hiyo.

Amesema Majambazi hao walikuwa na lengo la kumpora fedha Neema baada ya kufunga duka lake lakini hawakuweza kufanikiwa baada ya njama yao kuharibiwa na jeshi la Polisi na Juhudi za kuwatafuta zinaendelea ili waweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Pikipiki hiyo na silaha hizo zimehifadhiwa katika kituo cha polisi Wilaya ya Kahama.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post