MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI YAANZA KUSIKILIZA KESI YA KUPINGA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA ILIYOFUNGULIWA NA FREEMAN MBOWE, ZITTO KABWE NA WENGINE | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 19, 2019

MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI YAANZA KUSIKILIZA KESI YA KUPINGA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA ILIYOFUNGULIWA NA FREEMAN MBOWE, ZITTO KABWE NA WENGINE

  Malunde       Wednesday, June 19, 2019

Mahakama ya Afrika Mashariki imeanza kusikiliza kesi ya kupinga Sheria ya vyama vya siasa iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, Zitto Kabwe, Maalim Seif, Rungwe na Salum Mwalimu kwa niaba ya Vyama 8 vya upinzani Tanzania  wakiiomba EACJ isimamishe matumizi ya sheria hiyo hadi kesi ya msingi itakapoamriwa.


Katika kesi hiyo ambayo viongozi wa upinzani wanawakilishwa na Mawakili Fatuma Karume, John Mallya na Jebra Kambole wanaomba mahakama kusitisha sheria hiyo.

Wakili Karume  ameeleza majaji wa mahakama hiyo leo Jumatano Juni 19, 2019 kuwa sheria hiyo inakiuka mkataba wa jumuiya ya Afrika ya Mashariki katika masuala ya haki na demokrasia.

Amesema miongoni mwa upungufu katika shauri hilo ni kuzuia viongozi wa upinzani kutoa elimu ya mpiga kura bila idhini ya msajili wa vyama vya siasa, kuzuia walinzi binafsi wa vyama na kuingiliwa uhuru wa vyama

Majaji wa mahakama hiyo bado wanasikiliza maombi ya upinzani kutaka mahakama hiyo kutoa uamuzi wa dharura kuzuia baadhi ya vifungu vya sheria hiyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post