KAULI YA IGP SIRRO BAADA YA WATANZANIA 9 KUUAWA MSUMBIJI


Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amesema watanzania wapatao 9 wameuawa na wengine 6 kujeruhiwa nchini Msumbiji ambako walikwenda kujitafutia riziki.

Akiongea leo mkoani Mtwara eneo la mpaka wa Tanzania na Msumbiji amesema mauaji hayo yamefanyika Juni 26, 2019 ambapo pia watu wa Msumbuji kadhaa nao wameuawa.

''Waliofanya haya matukio tutawatafuta na nimeongea na IGP mwenzangu wa Msumbiji nimemuomba tukutane kesho Juni 30, 2019 ili tuongee juu ya tukio hili na mengine'', amesema.

IGP Sirro amesema amesikitishwa sana na vifo vya watanzania hao ambao wamepigwa risasi na watatumia kila njia kuwapa waliofanya mauaji hayo.

Pia ametoa pole kwa familia zilizopoteza ndugu zao pamoja na majeruhi 6 walionusurika kwenye mauaji hayo. Amewataka wananchi watoe taarifa zinazoweza kusaidia kupatikana kwa wauaji hao.

Imeelezwa kuwa watanzania hao huenda nchini Msumbiji wakati wa msimu wa kilimo kwaajili ya kulima na kujipatia mazao pamoja na kipato.
 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post