WATANZANIA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA MIFUKO MBADALA


Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuchangamkia fursa ya kutengeneza mifuko mbadala kwa kuwa mahitaji ni makubwa na soko ni kubwa.

Majaliwa amesema hayo jana Ijumaa Juni 28, 2019  wakati akitoa hoja ya kuahirisha kikao cha mkutano wa 15 wa Bunge la Tanzania.

Amesema uzalishaji wa mifuko hiyo hautoshelezi mahitaji kwa sasa.

Majaliwa amesema utekelezaji wa katazo la Serikali ya Tanzania la mifuko ya plastiki limefanikiwa kwa kiasi kikubwa, wananchi wameonyesha mwitiko wa hali ya juu kutumia mifuko hiyo.

Amesema jumla ya viwanda 11 vimejikita kwenye uzalishaji wa mifuko mbadala 10 vikiwa Dar es Salaam na kimoja Arusha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527