BODI MPYA JATU PLC YASHAURIWA KUFANYA KAZI KWA BIDII


 Mgeni rasmi,katika mkutano Mkuu wa JATU,Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshugulikia masuala ya ajira, Vijana na walemavu, Eliachimu Mtawa  akizungumza mbele ya wageni waalikwa katika mkutano huo uliofanyika hivi karibuni jijini Dar

 Mkurugenzi wa Jatu PLC Peter Isare,akizungumza mbele ya Wageni waalikwa waliofika kwenye mkutano huo,ambapo ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ni ya umma kwani inawanachama zaidi ya 13,0000 na Agosti mwaka huu wataingia Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) kwa mtaji wa Sh.bilioni 7.5.Pia akafafanua zaidi kwa wanachama wapya kuwa Kampuni hiyo  ilianzishwa na vijana 2015 .
Pichani nyuma ni wajumbe wa bodi mpya ya Jatu PLC walioteuliwa kwenye mkutano huo na Wanachama wao.
Baadhi ya Wanachama wa Kampuni ya JATU wakifuatilia mkutano . 
 Mmoja wa Wanachama wa JATU akiuliza swali kwa Uongozi wa kampuni hiyo akitaka ufafanuzi wa baadhi ya jambo kuhusiana na MKutano huo. 
Picha ya pamoja
***
SERIKALI imeitaka bodi mpya ya Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umaskini (Jatu PLC), inafanya kazi kwa bidii na kuitendea vema dhamana waliyopewa.

Hayo yamesemwa na Ofisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshugulikia masuala ya ajira, Vijana na walemavu, Eliachimu Mtawa ambapo amesema anafurahi kuona Jatu hapa ilipofika kwani anaifahamu tangu mchakato wake wakati wanaanza.

"Nakumbuka walikuwa wakuja ofisini na maombio yao"Proposal), tunarekebisha, tunawashauri, wanaenda wanarudi lakini mwisho tuliwasapoti na leo ni kampuni kubwa, ofisi ya Waziri mkuu inajivunia katika hili,"amesema.

Ameongeza kuwa dhamana ambayo wamepewa ni kubwa hivyo ameshauri wahakikishe wanaitendea haki na Ofisi ya Waziri Mkuu kama walezi wa Jatu, watafuatilia kwa karibu.

Mtawa amesema mnyororo wa kilimo ni Mona ya juhudi zinazoweza badilisha maisha ya mtu na kuwataka wasikubali kuyumbishwa na kurudi nyuma kwani kuranya hivyo watakua wameikosea ofisi ya Waziri Mkuu na hata nafsi zao zitawasuta.

Wakati huo huo waliopitishwa kuwa wajumbe wa bodi mpya ya Jatu PLC ni Abdallah Gonzi, ambaye ni Mwalimu wa Sheria Chuo Kikuu Cha Dar e s Salaam (UDSM), Mhandisi Zakia Yona, Ian Semakande ambaye ni Mhasibu Finias Upanga, Noel Kaganda na Mwajuma Hamza.

Awali, akizungumza wakati akifungua mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva amesema Jatu inapoelekea soko la hisa ni vema wakafuata Katiba yao na kuhakikisha hawapokei mnung'uniko yeyote kutoka kwa wanachama.

"Kampuni inaingia katika soko la hisa ni jambo zuri kwani mnaondoa umaskini lakini hakikisheni hakuna manung'uniko, kupitia mkutano huu mkuu wanachama kwa kauli moja tuseme tunataka kwenda huko katika soko la hisa," amesema.

Lyaniva amesema ni vema kukawa na uwazi na umakini katika masuala ya mapato na matumizi ya jatu na yasomwe iwe wazi yanasomwa kwa utaratibu waliojiwekea kwa mujibu wa Katiba.

"Mfate katiba yenu inasema nini, mkae na kuzungumza vipaumbele vyenu pia muweke uwazi katika masuala yenu kwa wanachama lazma menejimenti iwe wazi kwa sababu mnatoka katika wazo moja kwenda lingine la kuingia katika soko la hisa na sasa kampuni itakuwa sio ya mtu binafsi ni yenu wote," amesisitiza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jatu PLC Peter Isare, ameishukuru Serikali kwa ushirikiano na kusisitiza kampuni hiyo ni ya umma kwani inawanachama zaidi ya 13,0000 na Agosti mwaka huu wataingia Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) kwa mtaji wa Sh.bilioni 
7.5.

Akizungumzia kampuni hiyo kwa wanachama wapya Isare amefafanua ilianzishwa na vijana 2015 kuhusiana na masuala ya afya na lishe na haki za binadamu, watu wengi wanapata changamoto kwenye masuala mbalimbali, 

"wengi ni maskini wanashindwa kumudu gharama za maisha na kusababisha migogoro kwenye jamii,"alisema na kuongeza "Tuwe na afya lakini tuweze kujitegemea na kuwa na afya nzuri, tumejikita kwenye kilimo, masoko na bima ya afya, watu wengi wanahitaji kuwekeza katika biashara na kuhitaji mikopo".

Pia amesema kampuni hiyo ya umma imesajiliwa mwaka 2016 na imefanikiwa katika kilimo cha mpunga Kilombero, Manyara kilimo cha alizeti na Mahindi, Tanga kulimo cha Maharage.

"Tunawawezesha wakulima kulima kilimo cha kisasa, na kuwapatia wataalamu ambao watawapa elimu, na kilimo ni cha muda wote kisichotegemea hali ya hewa. Igima kiwanda cha kukoboa mchele, Kibaigwa kiwanda cha mahindi na alizeti, tunaunganisha kilimo na viwanda, na soko tumelitengeneza wenyewe,"amesema.

Ameeleza Jatu unaponunua chochote kama chakula, ni rahisi kukuza faida Kwani kuna mfumo rasmi wa kugawa faida, mteja akinunua bidhaa anapata bonasi ambapo gawio analipata mwisho wa mwezi.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post