IRAN YAKUTANA NA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI KUOKOA MAKUBALIANO YA NYUKLIA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 28, 2019

IRAN YAKUTANA NA MATAIFA YENYE NGUVU DUNIANI KUOKOA MAKUBALIANO YA NYUKLIA

  Malunde       Friday, June 28, 2019

Wanadiplomasia wa ngazi ya juu kutoka mataifa matano yaliyo na nguvu duniani wanakutana na wenzao wa Iran mjini Vienna Austria, katika juhudi za kuishawishi Tehran kutoachana na makubaliano ya pamoja ya nyukilia. 

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araqhchi amewaeleza waandishi wa habari mjini Vienna kuwa Uingereza, Ujerumani na Ufaransa wanapaswa kuwasilisha mipango thabiti ili kupunguza athari za vikwazo vya Marekani. 

Mataifa hayo ya Ulaya yanatarajia hii leo kuwasilisha mpango wa biashara baina yake na Iran unaojulikana kama Instex, ili kuepuka vikwazo vya Marekani. 

Hata hivyo kuna wasiwasi kuwa mpango huo huenda usifufue mauzo ya mafuta ya Iran kwasababu makampuni na wafanyabiashara wana hofu kuwa mkataba wowote na Iran utawafanya walengwe na Marekani katika hatua zake. 

Marekani ilijiondoa katika makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa mwaka 2015 na kuiweka vikwazo vipya Iran vinavyolenga sekta ya mafuta ya taifa hilo la Kiislamu.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post