DIEGO MARADONA AMCHANA MESSI



Diego Almando Maradona amesema kuwa Kapteni wa timu ya taifa ya Argentina mbaye pia ni Kapteni wa klabu ya Barcelona, Lionel Messi kuwa hafai kuwa kiongozi wa timu hiyo.


Akiomtolea mfano hasimu wake na Messi, Cristiano Ronaldo amesema anavyomuangalia Ronaldo anavyopambana na timu yake ya Taifa (Ureno) utagundua kuwa ni mtu mwenye sifa za kuwa kiongozi anawapa wenzake ari ndani na nje ya uwanja tofauti na Messi.


“Ronaldo atabaki kuwa ni kiongozi na mchezaji wa mfano, Angalia anavyopambana akiwa uwanjani na hata anavyokuwa na wenzake, yule ni kiongozi. Messi hafai kuwa kiongozi na hana haiba hiyo kwa wachezaji wenzake wa Argentina. Natumaini siku moja Ronaldo atakuja kuichezea Argentina.“amesema Maradona kwenye mahojiano yake na ESPN muda mchache baada ya mchezo huo.


Jana usiku michuano ya Copa America imeendelea ambapo kulikuwa na mchezo wa kukata na shoka kati ya Argentina dhidi ya Colombia, ambapo Argentina walikubali kichapo cha goli 2-0.


Kwa matokeo hayo ya mchezo wa kwanza, Colombia wanaongoza kundi B huku Argentina wakishika mkia, timu nyingine kwenye kundi hilo ni Paraguay na Qatar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post