Mzee wa miaka 77 nchini Kenya amekutwa amefariki dunia kwenye chumba cha anasa baada ya kukesha na mwanamke mmoja ambaye bado hajatambuliwa.
Babu huyo aliyejulikana kwa jina la Robert alipatikana uchi wa mnyama kwenye kitanda alichokuwa amejistarehesha na mtoto huyo wa kike.
Wahudumu kwenye hoteli ya Kajiado ambapo alipatikana mzee huyo walisema alifika hapo Jumapili, Juni 9,2019 mida ya saa tisa hivi na baada ya kunywa chupa kadhaa za kileo akamchukua mrembo huyo na kuingia kwenye chumba cha malazi.
Haikubanika kilichofanyika chumbani humo ingawa kulikuwa na dalili za mzee huyo kushiriki penzi na mpenzi wake kwani maafisa wa polisi walipata mipira ya ngono iliyok
Mzee mwenyewe hakuwa na majeraha yoyote huku maafisa wakianza kumsaka binti aliyeingia mitini ili wajue kilicho sababisha mzee kukata roho.
Mwili wa simba huyo mkongwe ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City huku ukisubiriwa kufanyiwa upasuaji.
Chanzo - Tuko