BAADA YA KUSOTA MAHABUSU..WEMA SEPETU ARUDISHIWA DHAMANA,MAHAKAMA YAMPA ONYO

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
BAADA ya kusota Mahabusu kwa siku saba hatimae leo Juni 24, 2019 Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemrudishia  msanii wa Bongo Movie nchini Wema Isack Sepetu  dhamana na kumuonya kutorudia tena kukiuka masharti ya dhamana ama sivyo mahakama haitasita kumfutia kabisa dhamana hiyo.

Uamuzi huo umesomwa leo Juni 24, 2019 na Hakimu Mkazi Maira Kasonde kufuatia Wema kutokuhudhuria mahakamani hapo Mara mbili bila kuwepo kwa  taarifa yoyote kutoka kwake wala kwa mdhamini wake.

Kufuatia ukiukwaji huo wa msharti, mahakama ilitoa hati ya kumkata Wema ambapo Julai 17 mwaka huu, alijisalimisha mahakamani hapo na Hakimu Kasonde akatoa amri kuwa mshtakiwa aende Mahabusu ambapo amekaa mahabusu katika gereza la Segerea mpaka leo

Akisoma uamuzi huo, amesema Juni 17, mwaka mshtakiwa Wema alifika mahakamani hapo chino ya hati ya kukamatwa  ili kuonyesha kwa nini dhamanana yake isifutwe . msando alifaili mahakamani hapo kiapo kikionyesha sababu za mshtakiwa kutokufika mahakamani Juni 11, mwaka huu ambapo alieleza kuwa mshtakiwa aliugua ghafla akiwa katika viunga vya mahakama na akashindwa kuingia ndani na kuamua kuondoka.

"Baada ya kufikiria kwa makini sababu za mahakama zilizotolewa na mshtakiwa katika hati ya Kiapo mahakama inaona kuwa kweli mshtakiwa alikiuka masharti ya dhamana, lakini kama binadamu hali inaweza kumtokea mtu yeyote lakini kwa nini hakuitaarifu mahakama wakati akiwa katika eneo hili?, amehoji Hakimu Kasonde.

Amesema, pale ambapo mshtakiwa haupo mahakamani unatakiwa kuijulisha mahakama kupitia mdhamini wako na kwa ba siyo kupitia wakili kwani wakili hachukui jukumu la mdhamini na kama mdhamini anashindwa kutoa taarifa mahakamani, inamaana mdhanini hiyo hafai na dhamana ya mshtakiwa inatakiwa kufutwa kabisa.

Wema anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza  video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani ambapo anadaiwa  kati ya Oktoba 15, 2018 katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam, alisambaza video za ngono kupitia akaunti yake ya Instagram, picha ambazo inadaiwa kuwa haina maudhui.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527