ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOMBA RUSHWA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, June 27, 2019

ASKARI WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA (JWTZ) AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOMBA RUSHWA

  Malunde       Thursday, June 27, 2019
Askari  wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), MT 77341 Johanes Kubambi, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) kwa shtaka la kuomba rushwa ya Sh 700,000.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Karoline Kiliwa, Wakili wa Takukuru, Vera Ndeoya, alidai kuwa katika ofisi za jeshi la akiba, Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa aliomba rushwa kwa Kelvin Fabian ili aweze kumpatia nafasi ya mafunzo ya jeshi.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Ndeoya alidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, hivyo aliiomba mahakama kutaja tarehe nyingine.

Hata hivyo, Hakimu Kiliwa alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao sio wanajeshi wala polisi na wawe na barua zinazotambulika kisheria, watakaotoa bondi ya Sh milioni 1 kila mmoja.

Mshtakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Juni 28 kwa ajilii ya kutimiza masharti ya dhamana.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post