AHADI YA RAIS MAGUFULI UJENZI WA BARABARA GEITA KUTIMIZWA

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Serikali imesema ahadi  ya  Rais Magufuli ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami  ya kutoka Kahama ,Bulyang’hulu   hadi Geita  yenye urefu wa  km   120 ipo palepale   na wakati wowote ujenzi unaweza kuanza.

Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.Elias Kwandikwa amesema hayo leo bungeni  jijini  Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa Busanda ,Mkoani Geita Lolensia Bukwimba aliyehoji juu ya ahadi mbalimbali za serikali juu  ya ujenzi wa  barabara  kwa kiwango cha lami ikiwemo barabara ya Kahama hadi Geita ,ni lini Serikali  itaanza kutekeleza ahadi hizo.

Katika majibu yake,Naibu waziri wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe,Elias Kwandikwa  amesema ahadi ya Rais  John Pombe Magufuli katika ujenzi wa Barabara mbalimbali hapa nchini ikiwemo barabara ya Kutoka  Kahama,Bulyangh’ulu,Bukoli hadi Geita  ipo palepale na ujenzi unaweza kuanza muda wowote kuanzia sasa.

Ikumbukwe  kuwa ,taratibu za kuomba kupandishwa  hadhi barabara zimeainishwa kwenye kanuni Na.43 na 44 za  mwaka   2009 za sheria ya barabara Na.13 Ya  mwaka  2007  ambapo  bodi ya mkoa  ya barabara  [Regional   Roads Boards] huwasilisha  maombi  kwa Waziri anayehusika na Barabara tajwa  kama itakuwa imekidhi vigezo  vya kupandishwa hadhi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527