AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTOA USHAHIDI WA UONGO

Na Amiri kilagalila-Njombe

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Njombe imemfikisha mahakamani bwana Osward evance Mbilinyi mkazi wa wilaya ya Makete kwa kutoa ushahidi wa uongo katika kesi ya hongo namba 2/2019 iliyokuwa ikiwakabili Christian batholomeo Sanga na Zabron Mwakagile iliyofunguliwa katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Makete.


Kwa mujibu wa takukuru mkoani njombe taarifa zinasema kuwa mshitakiwa akiwa ni shahidi wa upande wa jamhuri anadaiwa tarehe 27/2/2019 wakati wa kesi ya hongo dhidi ya Christian sanga na Zabron mwakagile mshitakiwa alitoa ushahidi wa uongo huku akikana kutotambua maelezo yake aliyoyatoa ofisini kwa hiari yake akiwa kama shahidi katika kesi hiyo ya hongo iliyokuwa ikimkabili Christian batholomeo sanga na Zabron mwakagile.

Katika kesi hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na mwanasheria wa takukuru baada ya mshitakiwa kutoa ushahidi wa uongo,mwendesha mashtaka aliomba mahakama kumtambua shahidi huyo kama shahidi aliyebadilika.

Kamanda wa takukuru mkoani Njombe Charles mulebya ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa umma kuwa wasikubali kurubuniwa na washtakiwa hasa pale ambapo wameamua kuungana na serikali katika vita dhidi ya rushwa kwa kutoa ushahidi wa uongo ili mshitakiwa aonekane hana hatia mbele ya mahakama kwa kuwa kufanya hivyo ni kuhujumu jitihada za takukuru katika mapambano dhidi ya rushwa.

Aidha katika hatua nyingine takukuru mkoani Njombe imemfikisha katika mahakama ya hakimu mfawidhi wilaya ya Makete Leuteli amanyise Malila ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi Ludihani kwa kutumia cheti cha mtu mwingine ambaye ni Festo amanyise Ngogo na kujipatia ajira kupitia cheti cha mtu mwingine.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527