AFCON 2019 : HAWA NDIYO ''WANYAMA'' WANAOSHINDANIA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA

Timu za soka barani Afrika na uhusiano wake na wanyama

Mashindano ya kuwania kombe la mataifa ya Afrika yanaendelea nchini Misri, huku nchi 24 zinazoshiriki - kila moja ikiwa na jina tofauti - zitakabiliana katika kipindi cha wiki zaidi ya tatu zijazo.

Majina ya bandia ya timu hizo yana maana kubwa kwa timu za Afrika zinazoshiriki -si kwa kuzipatia utambulisho kwa mashabiki wake , bali pia huwasaidia wachezaji kupata motisha.

Majina bandia ya timu, pamoja na mashabiki waliovalia nguo za rangi mbali mbali za kuvutia pamoja na ngoma ni vitu vinavyochangamsha shindano. 

Mwewe wanaopaa juu

Kwa kipindi cha wiki tatu zijazo huenda Kunguru wakawa maarufu zaidi nchini Misri.

Ingawa timu ya Nigeria ni maarufu kwa sare yao ya kijani kibichi, jina Tai wa Nigeria au (Super Eagles of Nigeria ) ni maarufu hata zaidi. Timu hiyo ilichukua jina hilo kutoka kwenye nembo ya taifa iliyo na kunguru

Timu yaTunisia inajulikana kama Carthage Eagles au Tai wa Carthage) kwasababu ya uhusiano wao wa kihistoria na ustaarabu wa watu wa mji wa kale wa Carthage , ambao nembo yao ya taifa ilikuwa ni Mwewe. Tunisia watataka kuona nguvu,na uwezo kutoka kwa wachezaji wao, tabia zote na mienendo ya mwewe.

Na usisahau Mwewe wa Mali (The Eagles of Mali).

Wakati huo huo Korongo wa Uganda (Uganda Cranes) watakuwa wanataka kupaa mwanzoni mwa mchezo wao.
Sauti za nyikani:

Ufalme wa dunia na nyikani

Kuanzia simba hadi nyoka,chui hadi ndovu, wote watakuwa katika shindano la mwaka huu, mkiwemo:

Cameroon - (Simba wasioshindwa)The Indomitable Lions: Ni jina ambalo kwa kweli limewafaa ikizingatiwa sifa na ukakamavu walionao uwanjani . Wameshinda kombe hilo mara mbili na wanatetea taji lao

Morocco - The Atlas Lions( Simba wa Atlas)
Senegal - The Teranga Lions(simba wa teranga)

Ivory Coast - The Elephants(ndovu): Jina hili linatokana na utajiri wa awali wa ndovu iliokuwanao Ivory Coast.

Benin - The Squirrels:(Nguchiro) Huyu akiwa ni mnyama mdogo kuliko wote katika orodha ya majina ya timu nyingine katika shindano la AFCON
Angola - Palancas Negras (Palahala mkubwa)
DR Congo - The Leopards(Chui)
Algeria - The Fennec Foxes(Mbwa mwitu wa Fennec)
Guinea-Bissau - The Djurtus (Mbweha)

Wafalme na Wapiganaji

Kuheshimu sheria ni jambo muhimu katika utamaduni wa Afrika - kwa hiyo haishangazi kwa timu hiyo kupata jina hilo .

Washindi wa mara saba wa kombe la AFCON- Misri ni wafalme wa Afrika na wana jina linalofanana kabisa na hadhi yao : Ma Pharaoh . Kikosi chao mwaka huu kinawajumuisha wachezaji kama Mo Salah, mshindi wa tuzo la Caf na la Mchezaji bora wa soka wa BBC wa mwaka.

Wafalme wa Championi Misri wana historia inayogusa wafalme wao

Ma Pharaoh wako katika kundi moja na Wapiganaji wa Zimbabwe (Warriors of Zimbabwe)

Kenya na Ghana, hata hivyo wamezipatia timu majina tofauti timu zao.

Harambee Stars ya Kenyalimetokana na neno la kiswahili lenye maana ya "kushirikiana kwa pamoja". Jina bandia linalotolea wito nchi na timu kushirikiana kwa pamoja kufikia lengo la pamoja.

Huku Ghanawakifahamika kama -Nyota weusi(The Black Stars) linatokana na nyota iliyopo kwenye bendera ya taifa. Nyota hiyo inaaminiwa na Shirikisho la soka la Ghana kuwa inainua umoja wa wachezaji.

mashabiki wa soka kote barani Afrika watakuwa na hamu kubwa ya kusunbiri mwisho wa mashindano tarehe 19 Julai ikiwa ni mwewe ndiye atakayepaa zaidi, simba au simba ndiye atakayeungurumaama mar pharaoh watakalia kiti cha enzi.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post