Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Kupokea Watalii 343 Leo

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo jioni Jumapili Mei 12  anatarajiwa kuwapokea watalii 343 kutoka China wanaokuja nchini kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kwa siku tano.

Mara baada ya watalii hao kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) itafanyika hafla fupi ya kuwakaribisha na kesho wataanza safari ya kutembelea vivutio  huku baadhi yao wakishiriki kongamano la uwekezaji sekta ya utalii litakalofanyika kesho.

Ujio wa watalii hao unatokana  Bodi ya Utalii (TTB) kuingia makubaliano na kampuni ya Touchroad International Holdings Groups ya China Novemba mwaka jana wakati wa ziara ya kutangaza utalii katika miji ya Beijing, Shanghai, Chengdu, Guangzhou na Hong Kongna nchini China.

Wanaowasili leo ni wafanyabiashara na watu maarufu, wawekezaji kutoka kampuni 27, waandishi wa habari 40, maofisa wa Serikali ya China na mawakala wa kampuni za utalii.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post