WANAFUNZI WAWILI SHULE SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA WATEULIWA KULIWAKILISHA TAIFA KONGAMANO LA DUNIA


Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Festo Mgina (kulia) akiwakabidhi bendera ya Taifa jana wanafunzi wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga kwa ajili ya wenzao wawili walioteuliwa kuliwakilisha Taifa katika kongamano la mazingira duniani linalofanyika nchini Finland nkushoto kwake ni mkurugenzi wa shule hiyo ambae ni mkuu wa msafara wa wanafunzi hao Kitova Mungai
**

Na Francis Godwin, Iringa 

Uongozi wa serikali ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umesema umepokea kwa heshima kubwa mwaliko wa wanafunzi wawili wa shule ya msingi Southern Highlands Mafinga ambao wamepata mwaliko wa kuliwakilisha Taifa nchini Finland katika kongamano la wanafunzi dunia wanaojali mazingira.

Akizungumza wakati akiwakabidhi bendera ya Taifa wanafunzi hao na kiongozi wao jana kwa niba ya serikali ya wilaya ya wilaya ya Mufindi mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Festo Mgina alisema kuwa heshima ambayo shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga imepata ni kubwa kwa wilaya ,mkoa na Taifa kwa ujumla. .
“ Huu ni mwaliko wa heshima kubwa kwa wilaya yetu na mkoa lakini kwa Taifa letu kualikwa katika kongamano kubwa kama hili la kujadili masuala ya mazingira duniani heshima hii sisi kama viongozi tunajivunia na tunapongeza shule kwa kuteuliwa kuwakilisha Taifa “ alisema Mgina.

Kuwa mwaliko huo umekuja wakati Taifa liko katika harakati ya kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hata kuanza mchakato wa kuondoa sokoni mifuko ya rambo ambayo ni moja ya vikwazo vya mazingira .

HIvyo aliagiza wakuu wa shule za msingi katika wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanafika katika shule ya Southern Highnalnds Mafinga ili kujifunza yale ambayo wanafunzi hao wawili watarudi nayo kutoka katika mkutano huo mkubwa nchini Finland.

“tunataka elimu na aagizo ambayo yatatolewa katika mkutano huo wa dunia nchini Finland vijana hao wakirudi basi kuweza kusambaza kwa wenzao kwenye shule zetu zote za Mufindi ikiwa ni pamoja na wakuu wa shule kufika kujifunza ili kila shule kuweza kujifunza elimu hiyo kwa faida ya mazingira ya maeneo yao “ alisema Mgina.

KIongozi wa wanafunzi hao nchini Finland ,mkurugenzi wa shule hiyo ya Southern Highnalnds Mafinga Kitova Mungai alisema kuwa shule hiyo ni miongoni mwa shule wanachama wa Klabu za mazingira duniani na kuteuliwa kwa wanafunzi hao kumetokana na ziara ya waratibu wa kongamano hilo ambao walifika kupema uwezo wa klabu zote nchini.

Hivyo baada ya kuvutiwa na jitihada zinazofanywa na klabu ya shule yake katika utoaji wa elimu ya mazingira na ufundishaji wa masomo ya ujasiliamali kwa wanafunzi ndipo wameweza kutuma mwaliko kwa wanafunzi wawili na kiongozi mmoja ambao watakwenda kushiriki kongamano hilo kwa muda wa siku 10 safari ambayo itaanza jumanne wiki hii.

‘’ Tunategemea kukutana na wawakilishi kutoka nchi mbali mbali duniani kama china ,Japan, Brazil ,Marekani ,China ,Uganda , Kenya na nchi nyingine nyingi ila tunaimani kubwa ya kuwakilisha vema Tanzania kwani watoto ambao wamechaguliwa kwenda katika kongamano hilo wanauwezo mkubwa sana katika elimu ya mazingira “ alisema Mungai.

Alisema watoto hao na wenzao wamekuwa mbele kuhifadhi mazingira ya Shule ikiwa ni pamoja na uoteshaji wa miche ya miti na kuipata shuleni hapo na majumbani kwao na kwao suala la uhifadhi wa mazingira ni shughuli yao ambao hata wakipewa nafasi ya kufundisha wenzao wamekuwa wakifanya vizuri.

Mungai alisema kuwa Tanzania ni imekuwa mbele katika vita dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi na kuwa hata mkakati wa serikali wa kuzuia mifuko ya rambo ni mkakati ambao wanafunzi hao wamekuwa wakifundishwa namna ya kutunza mazingira pasipo kutumia mifuko hatarishi ya mazingira na kuwa kupitia kongamano hilo watapata kuwasilisha mbinu mbali mbali za utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wao wanafunzi watakaowakilisha Taifa katika kongamano hilo Maria Wambura na Stephen Sanga ambao ni wanafunzi wa darasa la saba katika shule hiyo walisema kuwa kuteuliwa kwao katika kongamano hilo si nafasi ya bahati mbaya kwani wanauhakika wa kuliwakilisha vizuri Taifa katika kongamano hilo na kile ambacho watakipata watakuja kutumia kutoa elimu kwa wanafunzi wenzao nchini .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post