WHATSAPP SIYO SALAMA...WADUKUZI WAMEFANYA YAO

Wadukuzi wanaweza kuweka programu ya Sofware ya kuchunguza taarifa kwenye simu yako na vifaa vingine vinavyotumiwa kwa kutuma ujumbe wa WhatsApp, imethibitishwa.


WhatsApp, ambayo inamilikiwa kampuni ya Facebook, inasema wanaodukua walilenga "namna walizochagua " za watumiajina waliongozwa na "watumiaji wakuu wa mtandao ".

Udukuzi huo ulibainika siku ya Ijumaa.

Jumatatu WhatsApp iliwaomba watumia bilioni 1.5 wa mtandao huo kufungua upya app zao kama njia zaidi ya kuepuka udukuzi.

Shambulio hilo dhidi ya WhatsApp, lililogunduliwa mapema mwezi huu ,lilikuwa ni la kwanza kuwahi kuripotiwa katika gazeti la Financial Times.

Unawahusisha wadukuzi wanaotumia sauti ya WhatsApp kuzipigia simu wanazozilenga. Hata kama simu hizo hazitapokelewa tayari programu ya udukuzi huwa imewekwa ndani ya simu inayolengwa na mara moja ujumbe wa kumuonyesha mwenye simu kuwa aliitwa na simu fulani hutoweka mara moja kwenye orodha ya simu zilizokuita.

BBC inafahamu kuwa kikosi cha usalama wa WhatsApp kilikuwa cha kwanza kubaini udukuzi huo, na kushirikisha taarifa hiyo makundi ya kutetea haki za binadamu , makampuni kadhaa ya usalama na wizara ta sheria ya marekani mapema mwezi huu.

"Wadukuzi wana kampuni ya kibinafsi ambayo inaripotiwa kufanya kazi na serikali ambazo huwapatia mfumo wa udukuzi ambao huchukua udhibiti wa mfumo mzima wa simu ," ilisema kampuni Jumatatu katika mazungumzo na waandishi wa habariUvamizi huo wa mtandao wa WhatsApp ulibuniwa na kampuni ya usalama ya Israeli inayofahamika kama NSO Group

Imeripotiwa kuwa uvamizi huo wa mtandao wa WhatsApp ulibuniwa na kampuni ya usalama ya Israeli inayofahamika kama NSO Group, kampuni ambayo awali ilielezewa kama "cyber arms dealer".

Programu yake kuu ya software, Pegasus, ina uwezo wa kukusanya taarifa za siri kutoka kwa mlengwa, ikiwemo kuchukua data kwa kutumia kipaza sauti(microphone) na kamera na kukusanya taarifa za mahali alipo mtumiaji wa simu.

Katika taarifa yake kundi hilo lilisema kuwa : "NSO's technology ina kibali cha utendaji wake na imeidhinishwa na wakala wa serikali kwa malengo ya kukabiliana na uhalifu pamoja na ugaidi.

"Kampuni haitumii mfumo wenyewe, baada ya kupewa kibali na kuchunguzwa, ujasusi na watekelezaji wa sheria huamua namna ya kutumia teknolojia kusaidia kazi yao ya kuhakikisha kunakuwa na usalama wa umma. Huwa tunachunguza madai yoyote ya kuaminika ya matumizi mabaya ya data na ikiwezekana tunachukua hatua, ikiwemo kuzima kabisa mfumo.

" Hakuna namna yoyote NSO inaweza kuhusika katika utendaji au kutambua walengwa wa teknolojia yake , ambayo hutumiwa na ujasusi na wakala wa utekelezaji wa sheria. NSO isingeweza au haiwezi kutumia teknolojia yake tkwa haki zake kumlenga mtu yeyote au kampuni , wakiwemo watu binafsi ."
WhatsApp imesema ni mapema kujua ni watumiaji wangapi wameathiriwa na udukuzi huo, ingawa washukiwa wengi walilengwa kwa kiwango kikubwa.

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni za Facebook , WhatsApp inajumla ya watumiaji bilioni 1.5 kote duniani.
Chanzo - BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post