WAKALA WA VIPIMO (WMA) ILALA WAKAGUA MIZANI ZA KUPIMIA VYAKULA SOKO LA KISUTUBw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala akihakiki mizani ya kupimia vyakula katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam leo, kulia kwake ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo.

.............................................................................

Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo na maofisa wa WMA  wamefanya ukaguzi wa mizani za kupimia vyakula katika soko la vyakula Kisutu leo ili kujiridhisha kama walaji wanapata huduma zinazostahili wakati wanapofanya manunuzi kwa wafanyabiashara wa soko hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika soko hilo Bw.Evarist Masengo amesema ni kawaida ya Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya ukaguzi mara kwa mara katika masoko, vituo vya mafuta, taasisi na maeneo mbalimbali ambayo Taasisi hiyo imekuwa ikisimamia katika masuala ya vipimo kwa ujumla.

Ameongeza kwamba Soko la Kisutu ni soko ambalo wafanyabiashara wake wamekuwa wakizingatia masuala ya vipimo kwa kiwango kikubwa hivyo kuwafanya wanunuzi au walaji wa bidhaa zao kupata huduma za manunuzi zenye ubora wa vipimo uliozingatiwa.

Amesema mnunuzi yeyote anayenunua bidhaa lazima awe makini kuangalia mizani kama imekaguliwa kwa sababu wao wanapokagua mizani wanaweka alama ya stika ya Wakala wa Vipimo (WMA) inayoonesha mwaka na tarehe ambayo mizani huo ulikaguliwa ili kumtambulisha mnunuzi kwamba huduma anayopata kutoka kwa mfanyabiashara imekidhi viwango.

Amewaasa wafanyabiashara kuhakikisha mizani zao zinakaguliwa na kuwekewa stika ya Wakala wa Vipimo (WMA) ili kutoa huduma iliyohakikiwa na itakayompa mlaji mahitaji yake kwa ubora.

Maofisa wa Wakala wa Vipimo (WMA) wanafanyika ukaguzi katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam na maeneo mengine ikiwa ni maandalizi ya maadhimisho ya siku ya vipimo duniani yanayotarajiwa kufanyika Mei 20/ 2019 jijini Dar es salaam.
Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo (kulia) na Bw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala wa pili kutoka (kulia) wakihakiki mizani ya kupimia vyakula katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam leo.
Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa TBC Stanley Ganzel wakati akigfafanua mambo mbalimbali katika soko la vyakula la kisutu katikati ni Bw. Costantine Clement Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA)Mkoa wa Ilala.
Baadhi ya vyakula , mbogamboga na matunda vinavyopatikana katika soko la Kisutu jijini Dar es salaam.
Bi Mary Lazaro Mfanyabiashara wa matunda katika soko la Kisutu akihojiwa na waandishi wa habari katika soko hilo.
Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akimsikiliza Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Wakala wa Vipimo (WMA) wakati alipokuwa akimueleza jambo.
Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akihakiki mzani mkubwa katika soko la Kisutu kulia ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo.
Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo wa pili kutoka kulia akiwa na maafisa wenzake kulia ni Contantine Clement Afisa Vipimo (WMA) mkoa wa Ilala kutoka kushoto ni Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi na Irene John Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Umma Wakala wa Vipimo (WMA).
Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Malaki Nyangasi akihakiki mzani mkubwa wakati maofisa wa 
MAOFISA WA WAKALA WA VIPIMO (WMA) WAFANYA UKAGUZI WA MIZANI KATIKA SOKO LA KISUTU LEO
Wakala wa Vipimo (WMA) walipokagua mizani katika soko la vyakula la Kisutu leo.
Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari.
Makamu Mwenyekiti wa Soko la Kisutu Bw. Laurent Magali akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ukaguzi huo uliofanywa na Wakala wa Vipimo (WMA) katika soko hilo katikati ni Afisa Vipimo Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw.Malaki Nyangasi na kushoto ni Meneja wa Wakala wa Vipimo (WMA) Mkoa wa Ilala Bw. Evarist Masengo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post