TANZANIA KUFIKIA ASILIMIA 70 YA KUONDOA UHABA WA WATUMISHI KATIKA SEKTA YA AFYA


Na.WAMJW,Dodoma
Tanzania imeazimia kufikia asilimia sabini kutoka arobaini na nane ya uhaba wa watoa huduma za afya kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ifikapo mwaka 2022.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wakati akifungua kikao cha kujadili changamoto za rasilimali watu katika sekta ya afya kati ya viongozi kutoka Wizara ya Afya, Tamisemi pamoja na washirika wa maendeleo nchini.

Waziri Ummy amesema lengo la kikao hicho ni kujadili changamoto mbalimbali zinazohusu rasilimali watu ikiwemo ya upungufu wa watumishi, ajira, mafunzo pamoja na mahitaji ya watumishi kuanzia ngazi za zahanati hadi hospitali za wilaya nchini.

Amesema upungufu huo umetokana na ongezeko la miundombinu ambayo imewekwa na serikali ya awamu ya tano licha ya kazi kubwa iliyofanyika ya kuimarisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

”ingawa bado ipo changamoto ya rasilimali watu katika sehemu za kutoa huduma za afya nchini ambapo pengo ni takribani asilimia 52 kwa kila watumishi wa afya mia moja tunawahitaji watumishi arobaini na mbili”. Amesisitiza Waziri Ummy.

Aidha, etaja sababu nyingine ya upungufu wa watumishi wa sekta ya afya kuwa ni pamoja na ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hivyo inahitajika watoa huduma wa afya wengi katika kuwahudumia wananchi wenye matatizo hayo.

Hata hivyo Waziri Ummy amesema kikao hicho kitaweka mikakati ya pamoja na ya ubunifu ya kuona kunakuwa na maboresho ya uzalishaji wa wataalam wa afya na wale wanaozalishwa ni kiasi gani wanaweza kuajiriwa na kuwekwa kwenye utumishi wa umma hususan kwenye ngazi ya zahanati na hospitali za wilaya.

“Tutaweka ubunifu ambao utawawezesha mfano wauguzi kupatiwa mafunzo ya kutoa dawa za usingizi na hii ni kuona wanao uwezo wa kufanya kazi nyingine tofauti, kwa ujumla sekta ya afya nchini inaenda vizuri na nina amini kwa pamoja tunaweza kutatua uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527