RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO BODI ZA MISHAHARA NCHINI | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, May 1, 2019

RAIS MAGUFULI ATOA MAAGIZO BODI ZA MISHAHARA NCHINI

  Malunde       Wednesday, May 1, 2019
Rais Magufuli amesema haelewi sababu za bodi za mishahara nchini Tanzania kutokutana kwa maelezo kwani yeye hana tatizo na kuonya vikao vyao kutokuwa uchochoro wa kutumia fedha za Serikali vibaya.


Ameyasema hayo leo katika sikukuu ya wafanyakazi Mei mosi, maadhimisho hayo kwa Tanzania yamefanyika  katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

“Kwangu mimi hata wakitaka kukutana leo sina shida, sina tatizo namuagiza waziri mwenye dhamana kuhakikisha bodi hizo zinakutana lakini vikao vyao visiwe vichochoro vya kutumia fedha za Serikali vibaya,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Lazima nitoe angalizo hilo maana unaweza kusikia wameenda kufanya vikao Dubai lakini suala la kukutana na kujadili masuala mbalimbali kati ya wafanyakazi na yale yanayopaswa kutatuliwa mapema nasema kwa dhati sina tatizo mkutane.”


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post