RAIS MAGUFULI ATEKELEZA AHADI YAKE KWA WAKAZI WA SENGEREMA
Friday, May 10, 2019
Ahadi yaRais Dkt. John Pombe Magufuli kwa wakazi wa Kata ya Nyampande, Wilaya Sengerema mkoani Mwanza ya kuwaondolea adha ya upatikanaji wa maji imeanza kutekelezwa, baada ya Serikali kusaini mkataba na mkandarasi ili kutandaza mtandao wa maji ya bomba katika
Kata hiyo.
Mkataba huowa zaidi ya shilingi bilioni moja umesainiwa Mei 09, 2019 baina ya Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA) pamoja namkandarasi kampuni ya HALEM ya jijini Dar es salaam mbele ya Mkuu wa MkoaMwanza, John Mongella.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mkoani Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM Construction ya jijini Dar es salaam, Mhandisi Happy Lebe (kushoto), wakisaini mkataba wa utekelezaji mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema. Aliyesimama upande wa kulia ni Mwanasheria wa MWAUWASA, Oscar Twakazi na kushoto ni Meneja Vifaa kampuni ya HALEM, Steven Malima.
Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya HALEM, Mhandisi Happy Lebe wakikabidhiana mkataba wa utekelezaji wa mradi wa maji Nyampande wilayani Sengerema baada ya pande zote mbili kuusaini.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin