MUSUKUMA ATAKA WIZARA YA MAJI IONGOZWE NA MTU MWENYE ELIMU YA DARASA LA SABA


Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufu Musukuma (CCM), ameitaka Wizara ya Maji, iongozwe na mtu mwenye elimu ya darasa la saba kama yeye kwani maprofesa wameshindwa kazi.

Musukuma ameyasema hayo bungeni leo  wakati akichangia mjadala wa wizara hiyo, ambapo aliwataja mawaziri waliowahi kuwa mawaziri wa wizara hiyo ambao ni maprofesa.

“Mheshimiwa Spika, tuliwahi kuwa na maprofesa, Mwandosya, Magembe, sasa Mbarawa na Katibu Mkuu Kitila Mkumbo, sasa tujaribu na darasa la saba muone, mimi nitaziba mitaro yote na mtashangaa,” amesema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post