MENEJA WA WAKALA WA VIPIMO (WMA) BANDARINI AELEZEA UMUHIMU WA KUPIMA MAFUTA KATIKA HATUA MBALIMBALI


Bw. Peter Chuwa Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Bandarini akizungumza na waandishi wa habari leo katika ofisi za (WMA) zilizopo kwenye Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo wakati akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu vipimo vya mafuta kwenye Meli Kwenye Matanki ya kuhifadhia na kwenye maroli yanayosafirisha nishati hiyo hapa nchini na nchi mbalimbali. 

Bw. Peter Chuwa amesema kuna umuhimu mkubwa sana kupima mafuta katika hatua yoyote ile iwe kwenye meli , kwenye matanki na hata kwenye maroli yanayosafirisha ili walaji waweze kupata ujazo ulio sahihi kabisa na wauzaji pia wauze kwa viwango na vipimo vinavyostahili na vilivyothibitishwa.

Mei 20 mwaka 1875 makampuni kadhaa huko ufaransa yalikutana na kujadili kuhusu vipimo hivyo ambapo yalikipitisha kipimo cha ujazo wa mita baada ya hapo tarehe ya Mei 20 kila mwaka iliteuliwa kuwa siku ya vipimo na imekuwa ikiadhimishwa duniani kote, Siku ya Jumatatu Mei 20,2019 ya wiki ijayo maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salaam.
Peter Chuwa Meneja Wakala wa Vipimo (WMA) Bandarini akifafanua mambo mbalimbali wakati akizungumza na 
waandishi wa habari leo katika ofisi (WMA) zilizopo Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) Barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam leo kuhusu vipimo vya mafuta kwenye Meli 
Kwenye Matanki ya kuhifadhia na kwenye maroli yanayosafirisha nishati  hiyo hapa nchini na nchi mbalimbali. 
Mjasiriamali na Mbunifu wa mashine mbalimbali za kutengenezea sabuni Bw. George Butafwe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea katika karakana yake iliyopo (SIDO) jijini Dar es salaam kuhusu vipimo sahihi katika kila kitu unachokifanya, Butafwe amesema vipimo ndiyo kila kitu kwani hata wabunifu kama yeye hawawezi kubuni mashine bila vipimo "Lazima ujue kwamba mashine hii naitengeneza itazalisha sabuni katoni ngapi kwa siku, Nitatumia Mawese kiasi gani labda malighafi nyingine kiasi fulani kwa hiyo vipimo ndiyo kila kitu". 
Mjasiriamali na Mbunifu wa mashine mbalimbali za kutengenezea sabuni  Bw. George Butafwe akifafanua jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea katika karakana yake iliyopo (SIDO) jijini Dar es salaam akiielezea mashine ya kutengenezea sabuni aliyoibuni mbele ya waandishi wa habari. 
Mjasiriamali na Mbunifu wa mashine mbalimbali za kutengenezea sabuni  Bw. George Butafwe akifafanua jambo kwa mwandishi wa habari wa TBC wakati wanahabari hao walipotembelea katika karakana yake iliyopo (SIDO) jijini Dar es salaam leo.
Afisa Vipimo II, Joram Joshua akiwa melini kwa ajili ya kupima ujazo wa mafuta Bandalini kabla hayajaanza kushushwa kwenye meli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527