MASELE KUENDELEA KUPETA BUNGE LA AFRIKA...ASAMEHEMEWA


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeazimia kumsamehe Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Masele kufuatia kukutwa na hatia ya kulidharau Bunge huku Kamati ya Maadili ikipendekeza kufungiwa mikutano mitatu.

Uamuzi wa kumsamehe Mbunge Masele umependekezwa na Spika Ndugai baada ya kusomwa kwa hukumu ya Kamati ya Maadili iliyowasilishwa mapema leo asubuhi na Mbunge Almasi Maige.

Akizungumzia hukumu hiyo, Spika Ndugai alipendekeza bungeni Spika Wa Bunge kumsamehe Mbunge Masele, na kueleza kuwa amepokea taarifa ya Mbunge huyo kutaka kuomba radhi.

"Nitumie nafasi hii kuomba radhi kwa Viongozi wangu wote waliopata usumbufu katika sakata hili akiwemo Rais Magufuli, sikuchonganisha mihimili, bali nilikata rufaa baada ya Spika kuniandikia barua ya kunisimamisha bila hata ya kuniuliza lolote", amesema Masele.

Masele alikuwa akituhumiwa kwa makosa ya kulidharau Bunge na kudharau Mamlaka ya kiti cha Spika.

Masele aliposimama alitoa tuhuma mbalimbali akidai Ndugai amewasiliana na Rais wa PAP ili amng’oe nafasi yake ya makamu wa Rais na ubunge wa Bunge hilo. Masele pia ameikataa taarifa ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge iliyomkuta na hatia.

Masele alihojiwa na kamati hiyo Jumatatu Mei 20, 2019 akituhumiwa na Ndugai kwamba amekuwa utovu wa nidhamu pamoja na kutoa maneno ya kugonganisha mihimili.

Ndugai alilieleza Bunge Mei 16, 2019 kwamba kutokana na utovu huo wa nidhamu amesimamisha uwakilishi wa Masele PAP ambako mkutano wa Bunge hilo ulikuwa ukiendelea nchini Afrika Kusini na kuagiza mbunge huyo kurejea nchini.

Alisema mara baada ya kurejea nchini, Masele atahojiwa na kamati hiyo pamoja na kamati ya maadili ya wabunge wa CCM.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post