RAIS WA BUNGE LA AFRIKA (PAP) AKUTWA NA KESI YA KUJIBU TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO, UMOJA WA AFRIKA KUCHUKUA HATUA | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, May 16, 2019

RAIS WA BUNGE LA AFRIKA (PAP) AKUTWA NA KESI YA KUJIBU TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO, UMOJA WA AFRIKA KUCHUKUA HATUA

  Malunde       Thursday, May 16, 2019

Mheshimiwa Stephen Masele akiandika dondoo muhimu wa wakati wa kikao cha bunge la Afrika leo,Midrand,Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Hatimaye Kamati Maalumu iliyoundwa na Wabunge wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP) imetoa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Rais wa Bunge hilo,Mhe. Roger Nkodo Dang.Nkodo anatuhumiwa kwa unyanyasi wa kingono kwa watumishi wa kike walioko Makao Makuu ya PAP,matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo dani ya bunge hilo na unyanyasaji kwa watumishi wa ofisi hiyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa watumishi wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Maalumu  ya Uchunguzi,Jaji mstaafu wa mahakamani kuu ya kenya Mh Stewart Madzayo ametoa ripoti hiyo leo jioni katika kikao cha bunge kikiongozwa na Makamu wa nne wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Chief Charumbira.

Ripoti ya kamati hiyo imeonesha kuwa Rais wa PAP, Nkodo Dang amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo wabunge wa wameazimia kuikabidhi Umoja wa Afrika (AU) kwa ajili ya uchunguzi wa kina(forensic investigation)ambapo Rais huyo ametakiwa apishe ili uchunguzi uweze kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kutoka kwenye kikao cha bunge ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele amesema Kamati hiyo imefanya kazi nzuri.

“Kwanza Nimefurahi kwamba Kamati Maalumu iliyoundwa na Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya rais wa PAP anazotuhumiwa imefanya kazi vizuri”,

“Na mimi kama mkuu wa Utawala wa Bunge la Afrika na wafanyakazi wote wa PAP, nina wajibu wa kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi hususani wanawake ambao wanamtuhumu rais kwa kuwanyanyasa kingono zinalindwa”,amesema Masele.

 “Utafiti wa Kamati umethibitisha kuwa alifanya hivyo na yeye mwenyewe amekiri kuwa alifanya na ameomba msamaha,Bunge limeazimia asimamishwe kupisha Umoja wa Afrika ufanye uchunguzi wa kina”.

MSIKILIZE/MTAZAME HAPA AKIZUNGUMZA


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post