LUKUVI AWASIMAMISHA KAZI WENYEVITI WAWILI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewasimamisha kazi wenyeviti wawili wa mabaraza ya ardhi na nyumba wa wilaya za Karagwe na Kibaha kutokana na malalamiko aliyopokea.

Licha ya kuwasimamisha wenyeviti hao wawili, waziri  amewateua wenyeviti wa mabaraza 20 nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Mei 7, 2019 mkoani Dodoma, Lukuvi amesema huo ni mkakati wa kuimarisha mabaraza 97 yaliyopo nchini.

Amesema katika kusimamia nidhamu ya uendeshaji na usimamizi wa mabaraza hayo, amekuwa akipokea tuhuma nyingi za rushwa, utendaji mbaya na malalamiko ya wananchi kwa wenyeviti wa Karagwe na Kibaha.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post