Picha : ASKOFU MAKALA AFUNGUA RASMI SHULE YA KKKT MAKEDONIA ENGLISH MEDIUM SHINYANGA

Kanisa la kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria chini ya Usharika wa Makedonia uliopo Jimbo la Shinyanga,limezindua rasmi shule ya 'KKKT Makedonia English Medium' iliyopo Lubaga Mjini Shinyanga ambapo mgeni rasmi wa uzinduzi huo alikuwa ni Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala.

Uzinduzi huo umefanyika leo Jumapili Mei 12,2019 katika ibada takatifu iliyoongozwa na Askofu wa kwanza wa Dayosisi Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria Dkt. Emmanuel Joseph Makala.

Katika mahubiri yake Askofu Makala, amesema "Uendeshaji na utoaji wa huduma za kijamii kama elimu kwa jamii ni sehemu moja muhimu kwa kanisa la Mungu na ndiyo mambo muhimu tuliyoitiwa kuyafanya katika umoja wetu".

Katika risala yake, mwenyekiti wa kamati ya kikosi kazi Bwana Shuma amesema mchakato wa kuanzisha shule hiyo ulianzishwa mwaka 2015 chini ya mchungaji Helman Gacha aliyeleta wazo la kuanzisha kituo Day Care Center na wazo hilo lilipokelewa na kuanza kutekelezwa mara moja. 

Amesema baadaye usharika uliamua kununua kiwanja kwa ajili ya kuendeleza shule hiyo na kiwanja hicho kilipatikana maeneo ya Lubaga manispaa ya Shinyanga. Chini ya mchungaji Harlod Mkalo pamoja na mchungaji mwenza Mathias Masele waliamua kuongeza nguvu kazi ndani ya kamati ya kikosi kazi ili kuhakikisha mambo hayakwami.

Mwenyekiti wa kamati hiyo amesema wakati shule hiyo inaanzishwa rasmi ilianza ikiwa na wanafunzi wawili na walimu wawili na baada ya miezi mitatu idadi ya wanafunzi ilifikia 27.
Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akisoma maandiko wakati wa uzinduzi wa shule hiyo.
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala,wakuu wa majimbo pamoja na wachungaji wakiendelea na ibada ya uzinduzi wa shule ya Makedonia English Medium.
Askofu Dkt. Emmanuel Joseph Makala akijiandaa na ufunguzi.
Baada ya uzinduzi na uwekaji wakfu wa shule ya Makedonia English medium.
Askofu Dr Emmanuel Joseph Makala akiendelea na ufunguaji wa majengo ya shule hiyo.
Muonekano wa gari la shule ya Makedonia English Medium.
Muonekano wa gari ya shule ya Makedonia English Medium kwa ajili ya wanafunzi.
Baadhi ya walimu na wanafunzi wa shule ya Makedonia English Medium
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Makedonia English Medium
Mwonekano wa majengo ya shule ya Makedonia English Medium
Mwonekano wa majengo ya shule ya Makedonia English Medium

Picha zote na Isaac  Masengwa Masengwa Blog 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post