IRAN YAKATAA MAZUNGUMZO NA MAREKANI


Rais Hassan Rouhani wa Iran amekataa mazungumzo na Marekani, baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Iran itampigia simu na kuomba kufanya mazungumzo "iwapo na wakati watakapokuwa tayari". 


Iran na Marekani zimeendeleza vita vya maneno katika wiki za karibuni wakati Marekani ikiimarisha vikwazo na kile inachosema ni lengo la kuishinikiza Iran kufanya makubaliano mengine mbali na masharti ya mkataba wake wa nyuklia wa 2015.

Shirika la habari la serikali ya Iran limemnukuu Rouhani akisema kuwa hali ya sasa sio nzuri kwa mazungumzo na chaguo lao kwa sasa ni kuyakataa. 

Trump alisema jana kuwa Iran itakabiliwa vikali kama itajaribu kufanya chochote dhidi ya maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati. 

Alisema ripoti kuwa Marekani inajaribu kuanzisha mazungumzo na Iran ni za uwongo, lakini akaongeza kuwa Iran itawasiliana nao iwapo, ama lini watakapokuwa tayari. Rouhani amesema Wairan hawatawahi kumpigia magoti mnyanyasaji.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527